http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

CHELSEA YAIBWAGA MAN CITY STAMFORD BRIDGE FERNANDO TORRES ANG'ARA





Fernando Torres alifunga Bao la ushindi katika Dakika ya 90 wakati Chelsea walipoibwaga Manchester City Bao 2-1 Uwanjani Stamford Bridge na kuchupa hadi Nafasi ya Pili wakiwa Pointi 2 nyuma ya Vinara Arsenal.
Bao hilo la ushindi la Torres lilitokana na makosa ya Beki Matija Nastasic alierudisha Mpira kwa kichwa kwa Kipa wake Joe Hart ambae nae alikuwa akitoka Golini kuja mbele na kupishana na Mpira huo ambao ulitokewa na Torres na kuukwamisha wavuni.
Torres pia ndie alikuwa mpishi wa Bao la Chelsea la kwanza ambapo jitihada yake ilimfanya ampite Beki Gael Clichy na kumlisha Andre Schurrle aliefunga.
Sergio Aguero ndie aliefunga Bao la Man City kwa ufundi mkubwa na kuifanya mchezo uwe 1-1 na ndipo katika Dakika ya 90 Torres akawa Shujaa wa mchezo huo

TOTTENHAM nao walibuka na ushindi wa goli moja  kwa bila dhidi ya  HULL city
Penati ya Dakika ya 80 ya Roberto Soldado imewapa ushindi wa Bao 1-0 Tottenham walipocheza Uwanjani kwao White Hart Lane na Hull City.
Penati hiyo ilitolewa na Refa Michael Oliver kwa kuunawa Mpira Mchezaji wa Hull Ahmed Elmohamady.
Ushindi huu umeipandisha Tottenham hadi Nafasi ya 4 wakiwa na Pointi 19, Pointi 3 nyuma ya Vinara Arsenal.

SUNDERLAND 2 NEWCASTLE 1
Bao la Dakika ya 84 la Fabio Borini kwa mzinga mkali leo limewapa Sunderland ushindi wao wa kwanza kwemye Ligi Msimu huu walipoipiga Newcastle Bao 2-1 na kujinasua toka mkiani.

Sunderland walitangulia kufunga kwa Bao la Steven Fletcher la kichwa kutokana na krosi ya Adam Johnson.
Mathieu Debuchy akasawazisha kwa Newcastle baada ya Hatem Ben Arfa kupiga Mpira Golini.
Lakini Borini, akitokea Benchi, ndio aliwaua Newcastle kwa shuti la Mita 25.


Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget