FILIPPO INZAGHI, Lejendari wa AC Milan mwenye Umri wa Miaka 40, anaamini kabisa kuwa Masupastaa wa leo, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, hawawezi hata chembe kuigusa Rekodi yake ya kung’ara, kuwika na kuleta ushindi kwenye Fainali ya Kombe kubwa.
Filippo Inzaghi amedai Rekodi yake ya kupiga Bao kwenye Fainali kubwa haiguswi na haiwezi kuguswa na yeyote anaecheza sasa.
Kwenye Fainali za Makombe makubwa alizocheza, Inzaghi alipiga Bao 8 wakati akichezea Klabu Vigogo za Italy, Juventus na AC Milan.
Binafsi Lejendari huyo anasikia fahari Rekodi yake ya Mwaka
2007 ambapo alipiga Bao zote 2 zilizoiteketeza Liverpool kwenye UEFA CHAMPIONS LIGI huko Athens, Ugiriki.
Baada ya hapo, Inzaghi alipiga Bao walipocheza UEFA Super Cup na Sevilla na Bao 2 walipoibonda Boca Juniors kwenye Fainali ya Kombe la Dunia la Klabu.
-MSEMO WA KUMBUKUMBU:
SIR ALEX FERGUSON: “Filippo Inzaghi alizaliwa kwenye nafasi ya Ofsaidi!”
Filippo Inzaghi ameeleza: “Mwaka 2007, Kocha wa Milan, Carlo Ancelotti, alikuwa hana hakika nicheze mimi au Alberto Gilardino kwenye Fainali huko Athens na Liverpool, nilicheza na nikafunga Bao 2. Nikaja kufunga kwenye Fainali ya Super Cup dhidi ya Sevilla na Bao mbili dhidi ya Boca Juniors kwenye Fainali ya Klabu Bingwa Duniani. ”
Akasisitiza: “”Bao 5 kwenye Fainali 3, na hizo ni Fainali muhimu na tulishinda zote, Si Messi wala Ronaldo watafikia hilo. Hii ni Rekodi, itabaki kwangu!
Filippo Inzaghi alistaafu kucheza Soka Julai 2012 baada ya Miaka 21 kwenye Soka na sasa yupo San Siro akifundisha Vijana akiwa na Klabu ya AC Milan.
Post a Comment