http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

LIGI YA MABIGWA ULAYA CHELSEA YAUWA ARSENAL YALALA GOLI MBILI PALE ENGLAND

 TORRES SHEREHE MECHI 100 NA BAO 2!!
 UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, Usiku huu imeingia kwenye Mechi zake za Tatu kwa Makundi na Arsenal kubwagwa kwao Emirates kwa Bao 2-1 na Borussia Dortmund huku wenzao Chelsea wakiitwanga Schalke Bao 3-0 Nchini Germany na huko San Siro, AC Milan na Barcelona zilitoka Droo ya Bao 1-1.
ARSENAL 1 BORUSSIA DORTMUND 2
Robert Lewandowski alifunga Bao la Pili zikiwa zimesalia Dakika 8 Mpira kwisha baada kuunganisha Krosi ya Kevin Grosskreutz na kuipa Borussia Dortmund ushindi wa Bao 2-1 dhidi ya Arsenal Uwanjani Emirates.
Henrikh Mkhitaryan ndie alieifungia Dortmund Bao la Kwanza baada Aaron Ramsey kuupoteza Mpira karibu na boksi lakini Arsenal walisawazisha kwa Bao la Olivier Giroud kufuatia Krosi ya Bacary Sagna.
Hata hivyo, Arsenal watahisi uonevu maana Lewandowski alionekana kuwa na bahati kubwa kubaki Uwanjani bila Kadi Nyekundu baada kumpiga kiwiko Sentahafu wa Arsenal Laurent Koscielny  mapema kwenye Kipindi cha Pili.

SCHALKE 0 CHELSEA 3
Fernando Torres amesherehekea kuanza Mechi yake ya 100 akiwa na Chelsea kwa kufunga Bao mbili huko Germany walipoichapa Schalke 3-0 na kutua kileleni mwa Kundi E.
Bao la Tatu la Chelsea lilifungwa na Eden Hazard.

AC MILAN 1 BARCELONA 1
Uwanjani San Siro, AC Milan na Barcelona zilitoka Sare ya Bao 1-1 huku Robinho akiifungia AC Milan katika Dakika ya 9 na Lionel Messi kusawazisha katika Dakika ya 24.
FC Steaua Bucureşti 1 FC Basel 1
FC Schalke 0 Chelsea 3
Arsenal 1 Borussia Dortmund 2
Olympique de Marseille 1 SSC Napoli 2
FC Porto 0 Football Club Zenit 1
FK Austria Wien Club 0 Atlético de Madrid 3
Celtic FC 2 AFC Ajax 1
AC Milan 1 FC Barcelona 1

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget