http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

GHANA YAWAUWA MAFARAO WA MISRI GOLI 6-1

GHANA, wakichezwa kwao Baba Yara Stadium huko Jijini Kumasi, leo wameitwanga Egypt Bao 6-1 na kujiweka kwenye nafasi nzuri sana kwenda Brazil kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia.GHANA_v_EGYPT MAGOLI: Ghana 6 -Asamoah Gyan Dakika ya 4 -Wael Gomaa 22 [Kajifunga mwenyewe] -Waris 44 -Asamoah Gyan 54 -Sulley Muntari [Penati] -Atsu 89 Egypt 1 -Mohammed AbouTrika Dakika ya 41 [Penati] Asamoah Gyan ndie alieipa Ghana Bao la kwanza na kuchanja mbuga kwa Kiungo Michael Essien kulizaa Bao lao la Pili baada ya Beki wa Egypt Wael Gomaa kujifunga mwenyewe. Mkongwe wa Egypt, Mohamed Aboutrika, akawapa Bao moja kwa Penati lakini Majeed Waris akaifungia Ghana kwa kichwa na kufanya Mabao yawe 3-1 na Gyan kufungwa kwa kichwa pia na Bao kuwa 4-1. Kisha Sulley Muntari akafunga kwa Penati na Christian Atsu kuipigia Bao la 6 Ghana na kuwaacha wawe tayari wameichungulia Brazil kabla kurudiana na Egypt huko Cairo hapo Novemba 19. Marudiano: Jumamosi Novemba 16 18:00 Nigeria v Ethiopia 22:00 Senegal v Ivory Coast Jumapili Novemba 17 17:30 Cameroon v Tunisia Jumanne Novemba 19 19:00 Egypt v Ghana 21:15 Algeria v Burkina Faso

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget