http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

BARANI ULAYA HAPATOSHI NAFASI SABA KUGOMBANIWA BAADA YA ZILE MBILI KUCHUKULIWA NA ITALY NA WADACHI


BRAZIL_2014_BEST
ITALY, NETHERLANDS TAYARI WAKO BRAZIL BADO NAFASI 7….!!
WASHINDI WA PILI 8 BORA KWENDA MECHI ZA MCHUJO KUPATA 4!!
HUKO KANDA ya ULAYA tayari Italy na Netherlands zimetinga Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwakani kwa kumaliza Washindi wa Makundi yao na bado yapo Makundi 7 hayajatoa Washindi na huenda wakapatikana Ijumaa hii na Jumanne ijayo katika Mechi za mwisho.
Pamoja na Washindi hao 9 wa Makundi, pia zipo Nafasi 4 za kwenda Brazil ambazo zitapatikana toka Mechi 4 za Mchujo ambazo zitashindaniwa na Timu 8 zitakazomaliza katika Nafasi ya Pili Bora toka Makundi 9 ya Nchi za Ulaya.
                 DONDOO MUHIMU:
-DROO: Droo ya kupanga Makundi ya Fainali za Kombe la Dunia itafanyika huko Bahia, Brazil hapo Desemba 6.
-NCHI AMBAZO ZIMESHAFUZU: Brazil (Wenyeji), Argentina, Australia, Costa Rica, Iran, Italy, Japan, Netherlands, South Korea, United States
ULAYA
-Wenye uhakika kucheza Mechi za Mchujo: Belgium, Germany
-Wenye uhakika kumaliza Nafasi mbili za juu za Makundi yao: Bosnia and Herzegovina, Croatia, France, Greece, Spain (Mabingwa Watetezi wa Dunia)
-Wenye uwezo wa kushinda Kundi lao: England, Iceland, Israel, Montenegro, Poland, Portugal, Russia, Slovenia, Sweden, Switzerland, Ukraine
- Wenye uwezo wa kufika Mechi za Mchujo : Albania, Armenia, Austria, Bulgaria, Czech Republic, Denmark, Hungary, Norway, Republic of Ireland, Romania, Turkey
 
IFUATAYO NI TATHMINI YA KILA KUNDI:
KUNDI A
Ni Timu mbili tu zenye matumaini ya kutwaa ushindi wa Kundi na kufuzu moja kwa moja kwenda Brazil na hizo ni Belgium na Croatia na Belgium wako mbele ya Croatia kwa Pointi 5.
Ijumaa Belgium wanaenda Zagreb kucheza na Croatia na wanahitaji Sare tu ili kufuzu.
Croatia ni lazima wazifunge Belgium hapo Ijumaa  na Scotland Jumanne ijayo katika Mechi zao zilizobaki na hapo hapo kuombea Belgium wafungwe Nyumbani kwao katika Mechi yao ya mwisho iliyobaki.
Wakishindwa hivyo, Croatia wataomba waende Brazil kupitia Mechi za Mchujo.
KUNDI B
Italy wameshafuzu na ni Washindi wa Kundi wakiwa Pointi 7 mbele ya Bulgaria wanaofuatiwa na Denmark walio Pointi 1 nyuma na Pointi 3 mbele ya Czech Republic na Armenia.
Bulgaria watacheza Ugenini na Armenia kisha Nyumbani na Czech Republic huku Denmark wakiomba ushindi dhidi ya Italy na Malta uwafanye wakamate Nafasi ya Pili, na pengine, kwenda Mechi za Mchujo.
KUNDI C
Germany wako kileleni Pointi 5 mbele ya Sweden na Germany, ambao wako Nyumbani, wanahitaji Sare tu na Republic of Ireland ili waende Brazil.
Austria wako Pointi 3 nyuma ya Sweden na wakiifunga Sweden na kisha kuifunga Faroe Island watamaliza Nafasi ya Pili na pengine kwenda Mechi za Mchujo.
Ireland, ambao wako Pointi 3 nyuma ya Austria, ni lazima kwanza wazifunge Germany na Kazakhstan na kuomba Sweden wanafungwa Mechi zao zote mbili zilizobaki na Austria kufungwa na Faroe Island ili wao wawe na nafasi ya kumaliza Nafasi ya Pili, tena kwa ubora wa Magoli.
KUNDI D
Netherlands tayari wamefuzu kwenda Brazil na Hungary wako Nafasi ya Pili, Pointi moja mbele ya Turkey na Romania.
Ijumaa, Hungary wanaenda Ugenini kucheza na Netherlands na kumaliza na Andorra.
Turkey watacheza Ugenini na Estonia kisha Nyumbani na Netherlands.
Lakini, kati ya Hungary na Turkey, Romania ndio wenye Mechi mbili za mwisho laini kwani Ijumaa wako Ugenini na Andorra na kumaliza Nyumbani na Estonia.
KUNDI E
Katika Kundi hili ni Cyprus pekee ambao wameshatoka huku Switzerland wakiwa juu Pointi 5 mbele ya Iceland na kufuatia Slovenia, Norway na Albania ambazo ziko tofauti ya Pointi moja moja.
Switzerland, ambao wana ubora mzuri wa Tofauti ya Magoli, wanaweza kufuzu kwenda Brazil ikiwa watapata Pointi mbili kwenye Mechi zao na Albania, Ugenini, na Nyumbani na Slovenia.
Iceland ni lazima wazifunge Cyprus na Norway ili waweze hata kumaliza Nafasi ya Pili.
KUNDI F
Russia wanaongoza Kundi wakiwa Pointi 1 mbele ya Portugal na wanasafiri kwenda kucheza na Luxembourg na Azerbaijan huku Portugal wako Nyumbani kucheza na Israel na kisha Luxembourg.
KUNDI G
Ikiwa Bosnia and Herzegovina watashinda Mechi ya Nyumbani dhidi ya Liechtenstein na kisha Ugenini na Lithuania watafuzu kwenda Brazil.
KUNDI H
England wako kileleni Pointi 1 mbele ya Ukraine na Montenegro huku Poland wakifuatia Pointi 2 nyuma.
England wako Nyumbani katika Mechi zao zote mbili dhidi ya Montenegro na Poland na ushindi katika Mechi hizo ni Tiketi yao kwenda Brazil.
KUNDI I
Spain wako juu Pointi 1 mbele ya France na wamebakiza Mechi mbili huku France wana Mechi moja tu.
Spain wanahitaji Pointi 4 katika Mechi zao zote za Nyumbani dhidi ya Belarus na Georgia ili kujihakikishia kwenda Brazil.
France wanacheza Nyumbani Jumanne na Finland na pengine nafasi yao bora ya kwenda Brazil ni kupitia Mechi za Mchujo.source soka in bongoposted by skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget