http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

MICHU AMBADILI DAVID VILLA TAIFA SPAIN!

MICHUFOWADI wa Swansea City Michu ameitwa kwenye Kikosi cha Timu ya Taifa ya Spain kwa mara ya kwanza ili kumbadili David Villa ambae ameumia enka. Spain inatarajiwa kucheza Mechi za Kundi lake za kufuzu kwenda Brazil Mwakani kwenye Fainali za Kombe la Dunia dhidi ya Belarus na Georgia hapo Oktoba 11 na 15. Michu ni Mfungaji hatari wa Swansea City ambae Msimu uliopita alipiga Bao 22 kwenye Ligi Kuu England ukiwa ni Msimu wake wa kwanza kucheza Ligi hiyo na Msimu huu tayari ana Bao 5. David Villa ndie anaongoza kwa Ufungaji Bora kwa Timu ya Taifa ya Spain katika historia na Jumapili alilazimika kutoka kwenye Dakika ya 60 ya Mechi ya La Liga kati ya Timu yake Atletico Madrid ilipoifunga Celta Vigo Bao 2-1. Katika tamko lao, RFEF, Shirikisho la Soka la Spain, lilisema David Villa ameumia na hawezi kupona kwa wakati hivyo Kocha Vicente del Bosque amemteua Michu kuziba pengo hilo. Mbali kuitwa Michu, vile vile Kocha Vicente del Bosque amelazimika kumchukua Mchezaji wa Real Sociedad Inigo Martinez kumbadili Raul Albiol ambae nae ameumia. Spain wanahitaji Pointi 4 tu katika Mechi zao mbili zilizobaki ili kufuzu kwenda Brazil. KIKOSI KAMILI: MAKIPA: Iker Casillas, José Manuel Reina, Víctor Valdés MABEKI: Álvaro Arbeloa, Juanfran Torres, Gerard Piqué, Inigo Martinez, Sergio Ramos, Ignacio Monreal, Alberto Moreno. VIUNGO: Sergio Busquets, Mario Suárez, Xavi Hernández, Andrés Iniesta, Koke, Francisco Alarcón "Isco",Pedro Rodríguez, Jesús Navas, Cesc Fábregas. MASTRAIKA: Álvaro Negredo, Juan Manuel Mata, David Jiménez Silva, Michu

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget