http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

YAMEIBUKA MAPIGANO KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KIJIJI CHA MVUGWE WILAYANI KASULU MKOA WA KIGOMA

YAMEIBUKA MAPIGANO KATI YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KIJIJI CHA MVUGWE WILAYANI KASULU MKOA WA KIGOMA

Yameibuka mapigano kati ya wakulima na wafugaji katika kijiji cha Mvugwe wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la BENARD BONIFACE mkulima wa kijiji aliuawa kwa kuchomwa mkuki ubavuni na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafugaji na mtu mwingine
amejeruhiwa.
Kamanda wa polisi mkoa Kigoma FRAISSER KASHAI ameamesema chanzo cha mapigano hayo ni chuki ya wakulima kwa wafugaji hao kutokana na kitendo cha wafugaji kutoka mikoa ya Shinyanga na Simiyu kuvamia maeneo yao na kuharibu mazao.
Kamanda KASHAI ameiambia Clouds Fm mkoani Kigoma kuwa ili kufanikisha kufanya uharifu huo wakulima walitumia uwepo wa operesheni kimbunga ya kukamata wahamiaji haramu kwa kuanza kuwafukuza wafugaji hao kwa kuswaga mifugo yao na kuua baadhi ya mifugo hiyo jambo lililowakasirisha wafugaji na kuchukua hatua ya kutumia silaha kujihami.
Baada ya kutokea mauaji hayo Kamanda KASHAI amesema kuwa wakulima walijikusanya na baadaye kuvamia nyumba za wafugaji na kuzichoma moto ambapo jumla ya nyumba sita zilichomwa.
Hata hivyo Kamanda Kashai amesema kuwa katika tukio la pili hakuna kifo wala majeruhi kutokana na uchomaji moto huo na kwamba jumla ya wakulima 13 wa kijiji hicho cha Mvugwe wanashikiliwa na polisi wakituhumiwa kuhusika na uchomaji moto huo wa nyumba za wafugaji ulioathiri mali.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget