http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

TUME YA KUKUSANYA NA KURATIBU MAONI YA KATIBA MPYA IMEISHAURI SERIKALI


TUME YA KUKUSANYA NA KURATIBU MAONI YA KATIBA MPYA IMEISHAURI SERIKALI
Tume ya Kukusanya na kuratibu maoni ya Katiba mpya inayoongozwa na Jaji Mstaafu JOSEPH WARIOBA imeishauri Serikali kurudi nyuma na kukaa na makundi yote yanayokinzana katika mchakato wa Katiba ikiwemo vyama vya Upinzani ili kuwezesha kuendelea kwa mchakato wa Katiba mpya kukiwa na maridhiano.
Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji WARIOBA amesema mgawanyiko unapojitokeza katika baadhi ya hatua za mchakato wa Katiba mpya ni kiashiria kibaya cha kutopatikana Katiba Bora inayoendana na matakwa ya wananchi.
Jaji WARIOBA amevilaumu vyama vya siasa kuingiza maslahi yao katika mchakato wa katiba badala ya kujali maslahi ya wananchi ikiwemo kuingilia mabaraza ya katiba kwa kuwaelekeza baadhi ya wajumbe aina ya maoni ya kuyatoa kwenye mikutano ya mabaraza huku akiahidi kupatikana kwa katiba mpya kwa wakati uliopangwa.
Kuhusu sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya Katiba iliyopitishwa hivi karibuni na Bunge na kuzuka kwa vurugu za kihistoria kabla ya kupitishwa kwake baada ya Naibu Spika wa Bunge JOB NDUGAI kuamuru kutolewa nje ya ukumbi wa Bunge kwa kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani bungeni FREEMAN MBOWE Jaji WARIOBA amesema upo mkanganyiko mkubwa katika sheria hiyo kuhusu majukumu ya Tume.Kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya mwaka 2011 iliyopitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Novemba 2011, Katiba mpya inapaswa kuwa Tayari kabla ya Mwezi April mwaka 2014.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget