http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

majina ya washambuliaji watano wanaotarajiwa kurudisha mapema garama za pesa zilizotumika kuwasajili


TIMU 16 zitakazo shiriki Ligi ya Vodacom Tanzania bara zipo kwenye kipindi kigumu cha kupigana vikumbo kuwania wachezaji kwa ajili ya kuimarisha vikosi vyao.

Pindi usajili huo unapokamilika kila upande uliofanikiwa unakuwa ukijigamba kutoa kipigo inapokutana na timu pinzani na maneno mengi ya vitisho.
Lakini hofu kubwa kwa kocha au kiongozi aliyefanikisha usajili wa mchezaji huyo akihofu endapo mchezaji huyo asipofanya vizuri yeye ndiye muhusika mkubwa na anayestaili kubeba lawama.
Hapa chini Goal Tanzania inakuletea majina ya washambuliaji watano wanaotarajiwa kurudisha mapema garama za pesa zilizo tumika kuwasajili kwa timu za Ligi ya Vodacom Tanzania bara na kunusuru vibarua vya makocha ambao walipendekeza nyota hao kusajiliwa.
1.Donald Ngoma
Huyu ndiye mchezaji ghali kabisa wa Yanga aliyewaharimu mabingwa hao wa Tanzani bara Milioni 95 kukamilisha usajili wake akitokea FC Platinum ya kwao Zimbabwe.
Usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umbo refu na uwezo mkubwa wa kufunga mabao ulikuwa ni gumzo kubwa nchini kiasi cha kupambana kwenye vichwa vya vyombo mbalimbali vya habari kwa muda wa mwezi mmoja.
Ujio wake Yanga unanfanya kuwa mchezaji wa kwanza kwenye Ligi ya Tanzania kusajiliwa kwa pesa nyingi na hadi sasa ndiye mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa wa dola 7000 kwa mwezi huku Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi wa Simba wakifuatia.
Ngoma anapewa nafasi kubwa ya kufanya vizuri kutokana na rekodi yake nzuri aliyotoka nayo akiwa Platinum na hata kwenye timu yake ya taifa ya Zimbabwe na kudhihirisha hilo tayri nyota huyo ameanza kuonyesha kwamba anaweza kufanya kile ambacho kinatarajiwa kwani tayari ameifungia Yanga bao katika mechi yake ya kwanza iliyokuwa ya kirafiki dhidi ya KMKM.
Imani kubwa ya mashabiki inatokana na Yanga kuwa na wachezaji wengi wanaotengeneza nafasi na kupiga krosi kuliko timu nyingine yoyote kwenye Ligi ya Vodacom jambo ambalo kwauwezo alilokuwa nalo mchezaji huyo wanaamini atafanya vizuri.
2.Hamisi Kiiza
Hili siyo jina geni kwenye ligi ya Vodacom Tanzania bara lakini hata kwa mashabiki na wadau wa soka ambao wanaujua vizuri uwezo wa Kiiza raia wa Uganda abaye kwa sasa anarudi kucheza Tanzania akiwa na kikosi cha Simba ambao ni wapinzani wakubwa wa Yanga.
Kiiza amesajiliwa na Simba akiwa mchezaji huru baada ya kutemwa na Yanga msimu uliopita akidaiwa ameshuka kiwango lakini Simba wanaamini bado mchezaji huyo anauwezo wakuwasaidia kufanya vizuri na kuamua kumsajili kwa kumpa misimu miwili huku akiigarimu timu hiyo milioni 35.
Kiiza amebeba matumaini makubwa ya mashabiki wa Simba ambao wanaamini atafanya kama vile alivyokuwa Yanga kwa kuwafungia mabao na kuipa ubingwa timu hiyo ambayo haijawahi kumaliza angalau nafasi ya pili kwenye misimu mitatu iliyopita.
Huenda kazi hiyo ikawa nyepesi kwa Kiiza anayefahamika kwa uwezo mkubwa wa kufunga mabao ya kuvizia na hata yale ya juhudi binafsi na kutokana na kikosi cha Simba kwa sasa kukosa mshambuliaji tegemezi baada ya hatihati ya uwepo wa Mganda mwenzake Emmanuel Okwi ambaye ndiyo mfungaji bora wa timu hiyo msimu uliopita.
3.Rashid Mandawa
Mshambuliaji mpya wa Mwadui FC, ambaye msimu uliopita alichezea timu kongwe ya Kagera Sugar na kufunga mabao 10 kitu amacho kilimshawishi kocha Jamhuri Kiwelo ‘Julio’ kumsajili kwenye kikosi chake.
Mandawa anatarajiwa kuongoza mashambulizi ya Mwadui FC, na mashabiki wengi wa timu hiyo wameweka matumaini yao kwake wakiami ndiye mtu atakaye wapa furaha na kuiona timu yao ikitamba licha ya kwamba huo utakuwa ndiyo msimu wake wa kwanza kushiriki Ligi ya Vodacom.
Wachezaji kama Athumani Idd, Anthon Matogolo na Nizar Khalfan wanatarajiwa kuwa chachu ya mafanikio kwa Mandawa kwa sababu ndiyo viungo ambao wanatarajiwa kumchezesha mshambuliaji huyo ambaye kwa sasa ameitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.
4.Saad Kipanga
Kipanga mmoja wa washambuliaji chipukizi ambao msimu ujao anatarajia kuiepeperusha vyema bendera ya Maafande wa JKT Ruvu iliyopo chini ya kocha Fredy Minziro aliyekibadilisha kwa kiasi kikubwa kikosi chake akitaka ubingwa.
Minziro ameamua kumpa majukumu Kipanga baada ya kugundua uwezo wake mkubwa wa kufunga mabao aliokuwa nao tangu akiwa Rhino ya Tabora misimu miwili iliyopita lakini aliyumba baada ya kwenda Mbeya City ambayo nayo ilimtoa kwa mkopo kwa timu ya daraja la kwanza ya Panone FC.
Kipanga anatajwa kuwa ni mmoja ya washambuliaji atakaye kuwemo kwenye mbio za kusaka tuzo ya kiatu cha zahabu kwa kupambana na wakali kama Ngoma,Kiiza na wengineo watakao fanya vizuri kwenye ligi hiyo katika ufungaji wa mabao.
Kipanga katika kazi hiyo anatarajiwa kushirikiana kwa karibu na Samuel Kamuntu, ambaye msimu uliopita alikuwa kwenye kiwango cha juu katika kuifungia timu hiyo mabao sambamba na mkongwe Gaudence Mwaikimba.
5.Gideon Brown
MSHAMBULIAJI mpya wa Mbeya City Gideon Brown amesajiliwa na timu hiyo hivi karibuni akitokea Ndanda FC, ametua kwenye timu hiyo akibebeshwa najukumu mazito na kocha Juma Mwambusi kuhakikisha anaziba vyema pengo la Poul Nonga aliyekwenda Mwadui FC.
Bensoni ndiyo tumaini jipya kwa sasa kwa kocha Mwambusi na mashabiki wa timu hiyo ambao tangu ilipoanza kushiriki Ligi ya Vodacom, misimu miwili iliyopita wamekuwa karibu na timu hiyo kutokana na mwenendo mzuri hivyo mchezaji huyo anatakiwa kuhakikisha anaitendea haki nafasi hiyo.
Pamoja na uwepo wa mkongwe Themi Felix, lakini bado Brown aliyetua Mbeya City kwa dau la milioni 15, huku akiwa amebeba matumaini ya maelfu ya mashabiki na viongozi wa timu hiyo kuwa anaweza kulipa fadhila na kurudisha garama za pesa zilizotumika kumsajili.

Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget