KOCHA wa klabu ya Manchester United, Louis Van Gaal amemponda
winga wake Angel Di Maria kwa kosa la kupata kadi nyekundu katika mchezo wa
jana wa robo fainali kombe la FA dhidi ya washika bunduki Arsenal uliopigwa
katika dimba la Old Trafford
Winga huyo aliyevunja rekodi ya usajili nchini Uingereza alipata
kadi nyekundu baada ya kupewa kadi ya njano ya pili kwa kumsukuma mwamuzi
Michael Oliver huku akiwa na kadi ya njano ambayo aliipata muda huo huo kwa
kosa la kujiangusha baada ya kukabwa na kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey
Van Gaal alisema mchezaji huyo alikosa umakini mpaka akapata kadi
hiyo ambayo ilipelekea kuongeza ugumu wa mchezo na kufanya Arsenal kuongeza
kasi ya mashambulizi langoni kwa mashetani hao
"Di Maria anajua kuwa mchezaji haruhusiwi kumshika mwamuzi
lakini hakulijali hilo.Alikosa umakini katika hilo kwani nilizingumza kabla ya
mchezo kwamba kupata kadi nyekundu katika mechi kama hii ni rahisi sana ila
hajazingatia hilo. " alisema Van Gaal
"Pia kocha huyo amesema alisikitishwa na kiwango kilichooneshwa
na timu yake katika mchezo huo na sasa nguvu zote anazielekeza katika kuwania
nafasi ya kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao
Katika mechi hiyo ya robo fainali Arsenal iliibuka na ushindi wa
2-1, magoli ya Arsenal yakifungwa na Nacho Monreal na Danny Welbeck huku la
Mashetani hao likifungwa na nahodha wao Wayne Rooney
Hii ni mara ya kwanza kwa washika bunduki hao wa jiji la London
kuifunga Manchester United katika uwanja wa Old Trafford tangu wafanye hivyo
mwaka 2006
Baada ya kutinga hatua ya nusu fainali Arsenal watacheza na
mshindi kati ya Bradford City na Reading ambao wanataraji kucheza mechi yao ya
marudiano jumatatu ijayo baada ya kutoka sare ya 0-0 katika mechi ya kwanza
Post a Comment