http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

KAMA AUKUANGALIA FAINALI YA CAPITAL ONE ANGALIA MATUKIO YOTE HAPA


HATIMAYE ndoto ya Jose Mourinho kutwaa kombe la ligi ‘Capital One Cup’ imetimia usiku  huu uwanja wa Wembley mjini London.
Mourinho alibainisha kuwa fainali ya Capital One Cup ni muhimu kuliko fainali zote alizocheza nyuma, hivyo lazima ashinde.
Chelsea imeichapa Tottenham Hospurs mabao 2-0 katika mechi ya fainali ya kombe la ligi iliyomalizika usiku huu Wembley.


Bao la kwanza la Chelsea lilitiwa kambani na Jonh Terry katika dakika ya 45′.
Chelsea walikwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0.
Kipindi cha pili kilipoanza, mshambuliaji anayetumia nguvu na anasema hawezi kuacha kutumia staili hiyo kwani ndio imemuweka awe miongoni mwa washambuliaji hatari duniani,


 Diego Costa alifunga goli la pili dakika ya 56′.
Costa ambaye ametokea katika kifungo cha mechi tatu alionesha cheche na thamani yake kwa Chelsea.
Licha ya ushindi huo, Spurs ndio walicheza mpira mkubwa na walimiliki kwa asilimia 63 kwa 37 za Chelsea.
Hata hivyo Chelsea walikuwa wajanja kwani walipiga mashuti 5 yaliyolenga lango dhidi ya 2 ya watakutu wa London.




































Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget