http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Pambano la Floyd Mayweather na Manny Pacquiao kupigwa mey 2 mwaka huu




Hatimaye tarehe ya pambano la wakali wawili wandondi duniani Floyd Mayweather na  Manny Pacquiao lililokuwa likisubiriwa kwa hamu imetajwa na wawili hao sasa watashuka ulingoni May 2,2015 huko mjini Las Vegas nchini Marekani.
Hii imetibishwa usiku wa jana mara baada ya mkali huyo wa ngumi Floyd Mayweather kupost katika mitandao ya kijamii picha ya mkataba wa makubaliano kati yake na Pacquiao ambao ulikuwa umesainiwa na wawili hao.
Pambano hilo ambalo limekuwa likisubiriwa kwa miaka mingi na mashabiki wa mchezo huo duniani lina thamani ya dola za kimarekani milioni 250.
“Niliwaahidi mashabiki wangu kuwa pambano litakuwepo na leo nimewathibitishia,May 2 tutatengeneza historia mpya hivyo usikose ” alisema Mayweather.
“Kuwapa mashabiki kitu walichotaka kukiona ndiyo lengo kuu.Hili litakuwa ni tukio kubwa la kihistoria katika michezo.Mashabiki wa boxing na michezo duniani kote watashuhudia makubwa May 2,Mimi siku zote ni bora na pambano hili ni nafasi ya kuonesha ubora wangu na kufanya kile ninachoweza kufanya ambacho ni ushindi tu ” alisema Mayweather.
Aidha kwa upande mwingine Mfilipino Manny Pacquiao amesema kuwa amefurahi kupata nafasi ya kuwapa mashabiki kitu walichokisubiria kwa muda mrefu na wanastahili”
“Pambano hili ni kwa ajili ya mashabiki wote duniani waliokuwa wanata liwepo na pia kuleta furaha kwa wafilipino wenzangu ” alisema Pacquiao
Floyd Mayweather ameshinda mapambano yote  47 aliyowahi kucheza huku Pacquiao akipoteza michezo mitanno tu kati ya 64 aliyocheza mpaka sasa.
Pambano hili linasubiriwa kwa hamu na mashabiki mbalimbali duniani kote kutokana na wawili hao hawajawahi kukutana  hata mara moja ulingoni.
CHANZO SHAFFIH DAUDA
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget