http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

MABINGWA WA TANZANIA AZAM FC KUTUPA KARATA YAKE YA KWANZA LEO LIGI YA MABINGWA


MABINGWA wa Tanzania Bara, Azam FC leo wanaanza kampeni yao ya kuwania taji la kwanza la Ligi ya Mabingwa Afrika watakapokuwa wenyeji wa El Merreikh ya Sudan Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam.
Mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa, ni marudio ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame Agosti 20, mwaka jana Uwanja wa Nyamirambo, Kigali, Rwanda.
Dakika 90 ziliisha timu hizo zikiwa hazijafungana na katika mikwaju ya penalti Merreikh waliing'oa Azam FC kwa 4-3 na kwenda Nusu Fainali, baadaye Fainali hatimaye wakabeba Kombe.
Lakini siku hiyo, Azam FC ilipata pigo kubwa, mshambuliaji wake, John Bocco aliumia kipindi cha kwanza na kutolewa na akakaa nje hadi Januari alipoanza kurudi taratibu baada ya kutibiwa hadi Afrika Kusini.
 
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget