http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Kapteni John Komba afariki dunia leo kutokana na kushuka kwa sukari


Mbunge wa Mbinga Magharibi Mh. Kapteni John Komba
amefariki Dunia leo saa 10 jioni katika Hosptali ya TMJ
Mikocheni.


Kwa Mujibu wa mtoto wa Marehemu Bw. Jerry Komba
amesema kifo cha marehemu baba yake kimetokana na
ugonjwa wa kisukari ambapo amedai kuwa sukari ilishuka
ghafla akiwa nyumbani kwake Mbezi Beach Dar es
salaam.




"Ni kweli mzee amefariki dakika 50 zilizopita, alikuwa
nyumbani amekaa lakini sukari ilishuka ghafla na baadaye
kidogo alifariki" amesema Jerry Komba mtoto wa
marehemu.
Katibu wa mbunge huyo Bwana Gasper Tumaini amesema
kuwa mbunge huyo alikimbizwa katika hospitali ya TMJ
ambapo ndipo mauti yamemkuta.
Aidha Bwana Gaspaer Tumaini ameongeza kuwa mwili wa
marehemu umehamishiwa katika hosptali ya Lugalo jijini
Dar es salaam ambapo ratiba ya Mazishi bado
haijafahamika.
Mpekuzi imewatafuta Afisa habari wa Ofisi ya Bunge
ndugu Owen Mwandumbya, Mkurugenzi wa Mambo ya nje
na Elimu kwa umma bwana Jesse Mwakasyuka na katibu
wa Bunge Dkt Thomas Kashilila bila mafanikio kwa kuwa
hawakupokea simu
Labels:

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget