http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Masihara ya Toure yagharimu Liverpool


Kolo Toure 




Mlinda ngome mkongwe, Kolo Toure, alifanya makosa ya kiholela na kuwatunuku wenyeji West Bromwich Albion bao la kusawazisha kwenye sare ya 1-1 dhidi ya Liverpool katika uwanja wa Hawthorns Jumapili.
Bila ya yeyote karibu katika dakika ya 67, Toure alimuunganishia straika wa West Brom, Victor Anichebe, ambaye alikuwa wazi, nafasi murwa ya kufunga na mshambuliaji huyo wa zamani wa watanashari wao Everton alifyatua mkwaju uliomzidia kipa Simon Mignolet maarifa.
Toure alibaki mikono kichwani kwa aibu baada ya masiara yake kugharimu Liverpool ushindi ambao ungewawezesha kudhibiti nafasi ya nne.

Wageni hao walijitia kifua mbele katika dakika ya 24 pale Raheem Sterling na Luis Suarez waliposhirikiana kupeperusha krosi iliyotiwa kizimbani na Daniel Sturridge.
Hilo lilikuwa bao lake la saba katika mechi sita za Liverpool mtawalia huku akisherehekea lake la 50 katika ligi ya Premier.
West Brom walipanda hadi nafasi ya 17 na alama 23 kufuatia sare hiyo.www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget