http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Alex Oxlade-Chamberlain aiwezesha Arsenal kurudi kileleni mwa ligi


Alex Oxlade-Chamberlain 


Chipukizi wa Uingereza, Alex Oxlade-Chamberlain, alibuka shujaa pale magoli yake mawili yalipoongoza Arsenal kunyakua tena uongozi wa ligi ya Premier walipolaza Crystal Palace 2-0 Jumapili.
Mechi hiyo iliyosakatwa uga wa Emirates ilishuhusia wenyeji wakingatua Manchester City kileleni angalau mpaka Jumatatu ikiwa vingozi hao wa awali watafanikiwa kuchakaza Chelsea uwanjani wao wa Etihad
.
Arsenal wana alama 55 kutoka mechi 24 wakifuatiwa karibu na City (53) na Chelsea (50) huku Liverpool (47) wakikosa nafasi ya kudhibiti nafasi ya nne baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 na West Brom.
Palace, ambao wameimarika pakubwa chini ya utawala wa meneja wao Tony Pulis ulioanza Novemba, walisalia alama moja juu ya nafasi za kushuka daraja.
Oxlade-Chamberlain, akicheza kiungo cha kati badala ya pembeni kama ilivyo kawaida, alijivinjari na mchezo mzuri baada ya kurejea kutoka jeraha la muda mrefu.
Alifungua uongozi dakika ya 47 baada ya kuvisha kipa wa Palace kanzu kabla ya kuhakikishia klabu chake ushindi dakika ya 73 pale alipofunika kombora ndani ya neti baada ya kubadilisha pasi za moja-mbili na mwenzake Olivier Giroud.www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget