http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Cavani kukaa nje wiki tatu


Edison Cavani 




Nyota wa Paris St Germain, Edison Cavani, atakosa mchezo kwa muda wa wiki tatu kufuatia jeraha la paja.
Mshambuliaji huyo atalazimika kukosa mechi yao ya Champions League dhidi ya Bayer Leverkusen baadaye mwezi huu, msemaji wa timu hiyo alitangaza Jumapili.
Ilibidi Cavani atolewe uwanjani Ijumaa pale PSG waliwalaza Girondins Bordeaux 2-0 kwenye kivumbi cha in Ligue 1 na keshoye, alienda kufanyiwa uchunguzi zaidi wa kimatibabu.

Raia huyo wa Uruguay amefunga mabao 20 katika mechi 30 tangu kujiunga na miamba hao wa Ufaransa musimu huu kwa gharama ya juu zaidi katika historia ya Ligue 1 ya euro milioni 64.
Cavani pia atakosa nusu fainali ya League Cup dhidi ya Nantes Jumanne na kivumbi cha Ligue 1 ugenini Monaco wanawafuata katika nafasi ya pili kwenye msururu.
PSG watasafiri Leverkusen katika raundi ya 16 bora ya Champions League Februari 18 kabla ya kuandaa mechi ya marudiano Machi 12.www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget