http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Ramsey kukaa nje wiki sita


Aaron Ramsey 




Kiungo wa kati wa Arsenal Aaron Ramsey hatachezea klabu hiyo kwa wiki sita baada yake kupatwa na matatizo akiuguza jeraha lake la paja, meneja Arsene Wenger alifichua Ijumaa.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales wa umri wa miaka 23 alikuwa mmoja wa nyota wa klabu hiyo ya London msimu huu, lakini hajacheza tangu Desemba 26 kutokana na jeraha hilo.
Alikuwa amerejea kwenye mazoezi kamili mapema wiki hii, lakini akazidisha jeraha hilo, jambo lililomzuia kurudi mchezoni wakati wa sare ya Arsenal ya 2-2 ugenini Southampton Jumanne.
Kutokana na matokeo hayo, na huku Arsenal wakiwa wamepoteza uongozi wa Ligi ya Premia kwa Manchester City, Wenger amefichua kwamba atajaribu kununua difenda mpya kabla ya kipindi cha kuhama kwa wachezaji Januari kumalizika baadaye Ijumaa.
"Aaron Ramsey atakuwa nje kwa wiki nne hadi sita. Ninahesabu wiki sita,” Wenger alisema, kwenye nukuu zilizochapishwa kwenye akaunti rasmi ya Arsenal kwenye Twitter.
"Tunajaribu kuleta mtu mmoja wka sababu ya pigo hilo la Ramsey na marufuku ya (Mathieu) Flamini."www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget