| |
Wenger atapata pesa zaidi za kununua wachezaji majira ya joto baada ya klabu hiyo kutia saini mkataba mpya wa mavazi na kampuni ya Ujerumani ya Puma ambao utaanza Julai 1.
Afisa Mkuu Mtendaji Ivan Gazidis alitoa ishara kuu zaidi kwamba Mfaransa Wenger atakaa Arsenal, akidokeza kwamba wanakamilisha mkataba mpya.
“Tumekuwa daima tukimuunga mkono Arsene, bodi imekuwa nyuma yake sawa na (mmiliki) Stan Kroenke," Gazidis aliambia kikao cha wanahabari alipoulizwa kuhusu siku za usoni za meneja huyo ambaye mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu.
“Tuko pahala pazuri, na tuna furaha. Kama nilivyosema awali, Arsene ataongeza muda wake wa kukaa nasi na wakati muafaka ukifika tutatoa tangazo hilo,” akaongeza.
Wenger amekuwa meneja wa Arsenal tangu 1996 na amesaidia klabu hiyo kushinda mataji matatu ya Ligi ya Premia na vikombe vinne vya FA.
Hata hivyo, kumekuwa na kiangazi tangu 2005 ingawa Arsenal wameendelea kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mkataba wa Puma, wa thamani ya takriban pauni 30 milioni kila msimu, utasaidia Arsenal kushindana na klabu nyingine kuu Ulaya sokoni.
"Moja ya malengo yetu ya muda mrefu na kuongeza mapato yetu ya kibiashara na kuna sababu inayohusiana na soka ya kutufanya tufanye hivyo, ni kuweza kuwekeza katika kikosi chetu,” alisema Gazidis.
"Kwa hivyo, hili lina umuhimu mkubwa sana kuhusiana na kusonga mbele kwetu uwanjani na tunapotazama majira ya joto kuendelea mbele, meneja atakuwa na pesa,” akaongeza.
Puma walibandua Nike kama kampuni ya kutoa mavazi kwa Arsenal kwa mkataba ambao utaanza kutekelezwa Julai 1.
Klab hiyo ya London kaskazini, ikisaidiwa na kuimarishwa kwa mkataba wake na shirika la ndege la Emirates, ilivunja rekodi yake na kutumia pauni 42.5 milioni kununua Mjerumani Mesut Ozil mwanzoni mwa msimu.www.skychami.blogspot.com
Post a Comment