http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Mata huenda acheze dhidi ya Cardiff


Juan Mata 




Juan Mata huenda akachezea Manchester United mechi yake ya kwanza mabingwa hao watakapokuwa wakijaribu kufufua kampeni yao ya Ligi ya Premia dhidi ya Cardiff City uwanjani Old Trafford Jumanne.
Mhispania huyo wa umri wa miaka 25 aliandaa kikao chake cha kwanza na wanahabari kama mchezaji wa United Jumatatu tangu ahamie huko kutoka kwa Chelsea kwa ada ya £37.1 milioni mwishoni mwa wiki na ikatangazwa kwamba atavaa jezi Nambari 8.
Kununuliwa kwa Mata kumefufua matumaini ya kukwamua United ambao wako nambari saba kwenye ligi, alama 14 nyuma ya viongozi Arsenal na sita kutoka kwa eneo la kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Meneja David Moyes alisema Mata alishiriki mazoezi na wachezaji wenzake wapya na kwamba angeamua Jumanne kama atamchezesha kiungo huyo wa kati dhidi ya Cardiff wanaoshika mkia katika ligi.
Moyes aliongeza kwamba Wayne Rooney, Robin van Persie na Marouane Fellaini ambao wamekuwa nje kutokana na majeraha, wamerudi na wanafanya mazoezi, jambo ambalo linafufua matumaini ya klabu hiyo.

Raia huyo wa Scotland alisema ana furaha sana kumnunua Mata, akisema alikuwa na shaka kama klabu hiyo ingefanikiwa kumpata.
"Nina furaha kuu,” Moyes aliambia wanahabari. “Nilipata habari mwezi mmoja au miwili iliyopita kwamba ingewezekana lakini bado sikuamini kwamba tungefanikiwa.
“Tulipopata habari kwamba kulikuwa na uwezekano wa Juan kuweza kununuliwa tulijitokeza mara moja.”
Mata hajacheza tangu siku ya Mwaka Mpya, ambapo alionyesha kukasirishwa kwake na hatua ya kumuondoa uwanajni mapema wakati wa ushindi wa Chelsea wa 3-0 dhidi ya Southampton.
Mechi ya Jumanne itapelekea mchezaji wa zamani wa United aliyependwa sana Ole Gunnar Solskjaer akirejea Old Trafford kama meneja wa Cardiff, baada ya kuchukua pahala pa Malky Mackay mapema mwezi huu.
Raia huyo wa Norway alisema ataweka kando hisia licha ya kwamba ndiye aliyefunga bao la ushindi wakati wa fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 1999 dhidi ya Bayern Munich.
"Ni vigumu kusema kama nitakuwa nimejitenga,” aliambia gazeti la The Sun. “Huwezi kujua, wakati mwingine hisia hukuteka hata kama hutaki, kwa mfano unapotoa hotuba wakati wa harusi yako.
“Lakini mimi si mtu wa kuonyesha hisia sana na kwa hivyo sidhani kama litakuwa tatizo. Mimi sana sana ni mtaalamu kushinda mtu wa hisia.”
KUINULIWA KWA EVERTON
Everton, ambao wameinuliwa na hatua ya Leighton Baines kutia saini mkataba mpya wa miaka mine, watalenga kuwapita wapinzani wao wa eneo la Merseyside Liverpool kwenye kinyang’anyiro cha kujiaptia nafasi ya kucheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya watakapokutana uwanjani Anfield Jumanne.
Everton chini ya Roberto Martinez wamo nambari sita na alama 42, alama moja na nafasi mbili nyuma ya Liverpool.
Everton hawajashinda nyumbani kwa wapinzani hao wao tangu 1999 na difenda wa Liverpool Kolo Toure alisema wanahitaji kuendeleza rekodi hiyo ili kujipa nafasi ya kupumua.
"Sote tunajua kwamba ni mechi kubwa,” alisema Toure. "Itakuwa kali sana lakini tunahitaji kushinda.
"Tunataka kuwa katika nne bora. Tuko hapo kwa sasa lakini tutaendelea kukaa hapo tukishinda mechi hii.
"Everton wanafanya vyema kwa sasa na Tottenham wametukaribia. Lakini tunacheza vyema na kila mmoja anaangazia mechi vyema.
Arsenal huenda wamkose kiungo wa kati Jack Wilshere wakati wa mechi yao ya Jumanne ugenini dhidi ya Southampton ambao watakosa Dejan Lovren na Gaston Ramirez kutokana na majeraha ya kano za vifundo vya miguu.
Mechi nyingine za Jumanne zitashuhudia Norwich City wakiwa wenyeji wa Newcastle United, Swansea City wasakate gozi na Fulham nao Hull City watembelee Crystal Palace.www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget