http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Villa wachukua Holt kwa mkopo


Grant Holt 


Aston Villa wamemchukua straika Grant Holt kwa mkopo kutoka kwa Wigan Athletic kwa kipindi cha msimu kilichosalia, klabu hiyo ya Ligi ya Premia ilisema kupitia tovuti yake Jumanne.
Holt, ambaye alijiunga na mabingwa wa sasa wa Kombe la FA Wigan mwaka uliopita akitokea Norwich City, amejiunga tena na meneja wake wa zamani Paul Lambert.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 32, ambaye alifunga mabao 53 katika mechi 92 alizochezea Norwich, amechukuliwa na Villa kujaza pengo lililoachwa na Libor Kozak aliyejeruhiwa.
"Kumpoteza Libor kutokana na jeraha ni pigo kwetu, bila shaka. Nilipojua kwamba Grant alikuwa amewekwa sokoni nilitaka haraka kumchukua kwa sababu ataongeza nguvu na uzoefu katika kikosi chetu ambacho kwa jumla bado ni change,” Lambert aliambia avfc.co.uk.

"Ninajua yale anaweza kufanya na hilo ni muhimu.”

Villa wako nambari 11 katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza, alama tano kutoka eneo la kushushwa ngazi na wametatizika katika kufunga mabao msimu huu. Wamefunga mabao manane pekee nyumbani msimu huu.
"Kuweza kurudi tena katika Ligi ya Premia, hasa katika klabu kubwa kama Villa, ni jambo kubwa kwangu na fursa kwangu kufanya kazi tena na meneja wangu wa zamani na watu wake," Holt alisema.
"Sote tunafahamu kwamba hii ni klabu iliyo katika mpito lakini tunapiga hatua. Tuna vijana wengi wachanga kwenye klabu ambao wanafanya kazi nzuri na nina furaha kujiunga nao na kuweza kusaidia,” akaongeza.www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget