http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Stoke yasajili wawili dable Guidetti na Ireland


John Guidetti 




Stoke City wamekamilisha kupata saini ya straika wa Manchester City John Guidetti kwa mkopo na pia wakampata Stephen Ireland kwa mkataba wa kudumu kutoka Aston Villa.
Guidetti, 21, amechezea Sweden mara moja na alipata umaarufu akiwa na klabu ya Uholanzi Feyenoord kwa mkopo msimu wa 2011-12 ambapo alifunga mabao 20 katika mechi 23.
Alipelekwa City na meneja wa zamani Sven Goran Eriksson lakini ametatizwa na majeraha tangu arudi Manchester, na amecheza mechi moja pekee msimu huu katika League Cup.
"Tulitaka kujaribu na kuongeza njia zetu za kushambulia na John atatusaidia kufanya hilo,” meneja wa Stoke Mark Hughes aliambia tovuti ya klabu hiyo.

"Yeye ni mtu ambaye ukimuweka maeneo mazuri atatumia fursa ambazo atapata kwa sababu yeye kawaida ni mfungaji mabao,” Hughes akaongeza.
Ireland, 27, ambaye ni mchezaji wa zamani wa Manchester City amekuwa kwa mkopo Britannia Stadium msimu huu, ambapo amecheza mara 16 na kufunga mabao matatu.
"Stephen ni mchezaji soka mwenye kipaji na ameonyesha yale anayoweza kufanya tangu ajiunge nasi,” Hughes alisema. “Tunafurahishwa sana na hali kwamba amejiunga nasi sasa kwa mkataba wa kudumu.”www.skychami.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget