http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Seedorf asema atakuwa kocha AC Milan


Clarence Seedorf 




Nyota wa zamani wa Uholanzi na AC Milan Clarence Seedorf ndiye atakayekuwa kocha mpya wa klabu hiyo ya Serie A baada ya kutangaza kufika kikomo kwa uchezaji wake Jumanne.
Mholanzi huyo wa miaka 37, ambaye hajawahi kuwa mkufunzi awali, aliambia kikao cha habari kwamba amestaafu uchezaji soka. Aliondoka Milan na kujiunga na Botafogo ya Brazil 2012.
“Hii si kwaheri, tutakutana tena,” akasema katika uwanja wa Botafogo.
“Ujuzi na uzoefu niliopata mwaka huu mmoja na nusu nikiwa Botafogo utanisaidia katika kibarua change kinachofuata ambacho ni kuwa kocha wa Milan.”
Agenti wa Seedorf Deborah Martin alisema ametia saini mkataba wa miaka miwili na nusu kumrithi Massimiliano Allegri, aliyefutwa na Milan Jumatatu, kufuatia msususu wa matokeo mabaya zaidi akiwa na mabingwa hao mara saba wa Ulaya.

Seedorf alisema hakwua akipanga kustaafu lakini ofa hiyo kutoka Milan ilipomfikia, ilikuwa tamu sana kiasi kwamba hangeikataa.
"Uamuzi (wa kumfuta Allegri) ulibadilisha mambo,” Seedorf aliambia wanahabari. “Nilipigiwa simu nikiwa katikati ya kipindi cha mazoezi. Bila shaka, ni pahala nilipokaa miaka 10 ya maisha yangu na nina uhusiano wa karibu sana na rais wa klabu hiyo na kwa hivyo waliponiuliza singekataa.”
Hatua ya kumteua Seedorf, ambaye alifana sana miaka 10 aliyochezea Milan, ni kama kucheza karata ingawa ana umaarufu mkubwa katika klabu hiyo na atatua akiaminiwa sana na wengi.
Kiungo huyo wa kati alikuwa mchezaji wa kwanza kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya akiwa na klabu tatu tofauti - Ajax Amsterdam 1995, Real Madrid 1998 na AC Milan 2003 na 2007. Pia alichezea Inter Milan na Sampdoria.
Mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Uholanzi alishinda mataji mawili ya ligi na Kombe la Italia pamoja na mataji mawili ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya alipokuwa Milan, katika kipindi ambapo alitawazwa Kiungo Bora wa Kati wa Uefa 2007.
Milan kwa sasa wako nambari 11 katika Serie A baada ya kutpa uongozi wa mabao mawili na kushindwa 4-3 na timu ya Sassuolo iliyopandishwa ngazi majuzi katika mechi iliyochezwa Jumapili. Hilo liliwaacha alama 30 nyuma ya viongozi Juventus na alama 20 kutoka nafasi ya mwisho ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya inayoshikiliwa na Napoli.www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget