http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Vikombe tano havitoshi- Ribery

Franck Ribery 
Franck Ribery alikosa kutawazwa mshindi wa taji Ballon d'Or licha ya kusaidia timu yake ya Bayern Munich kunyakua mataji tano mwaka uliopita.
Nyota huyo ambaye alihusika pakubwa taifa lake Ufaransa kufuzu Dimba la Dunia la 2014, amesima hakuna lingine angefanya kutawazwa kama mchezaji bora duniani zaidi ya ufanisi wake mwaka uliopita.
Ribery alifuata Cristiano Ronaldo wa Ureno/Real Madrid na mtanashari wake Lionel Messi wa Argentina/Barcelona, kwenye orodha ya wachezaji tatu bora duniani mwaka jana.
Akiwa kigezo cha Bayern, Ribery na wenzake walishida vikombe vya Champions League, European Super Cup, Club World Cup, Bundesliga na DFB Pokal mwaka jana.
“Ni kipi zaidi nigefanya baada ya kushinda mataji hayo yote,” staa huyo aliambia jarida la Ujerumani, Bild, Jummanne.

"Haijalishi kama uko nafasi ya pili au tatu. Sina uchoyo lakini taji hilo si lengo langu.
“Nigependelea zaidi kushinda kila kombe na Bayern musimu huu na Kombe la Dunia. Hilo ndilo muhimu,” Ribery alizidi.
“Bila shaka, nigetamani kushinda lakini hakuna hoja.”
Mkurugenzi wa michezo Bayern, Matthias Sammer, alisema machoni mwake, Ribery ndiye nambari moja.
“Ni kura ya haki na tunafaa kutambua hivyo lakini kwetu sisi, hakuna aliye bora kama Franck,” Sammer aliambia maripota.www.skychami.blospot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget