http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Allegri afutwa kazi AC Milan


Enzi ya Masimilliano Allegri kama meneja wa AC Milan ilifikia kikomo Jumatatu huku miamba hao wa Italia wakijaribu kumshawishi kiungo wao wa zamani, Clarence Seedorf, kurithi wadhifa huo.
Seedorf bado ni mchezaji aliyesajiliwa na klabu cha Brazil, Botafogo, ingawa duru zinaarifu kuna kipengee kwenye kandarasi yake kinacho mruhusu kuwaaga iwapo nafasi ya kocha itatokea timu nyingine.

Shirika la habari la Italia, ANSA, limesema Botafogo wananuia kushikilia kiungo huyo maarufu hadi baada ya shindano la Marekani Kusini, Copa Libertadores, litakalo anza Januari 29.
“Ikiwa mnataka Seedorf, basi leteni Kaka na Robinho kucheza Libertadores,” rais wa zamani wa Botafogo, Carlos Augusto, ambaye anashikilia ushawishi mkubwa katika timu hiyo, alinukuliwa akisema.
Kaka na Robinho ni nyota wa Brazil ambao bado wanachezea AC Milan.
Kwa wakati huu, naibu wa kocha, Mauro Tassotti, ametwaa hatamu za uongozi huku taarifa zaidi Italia zikisema kuwa mshambuliaji wao wa zamani, Filipo Inzaghi, anaweza kujaza nafasi hiyo kwa muda.
Inzaghi ni mkufunzi wa kikosi chipukizi cha timu hiyo kwa sasa.
Allegri alipigwa kalamu baada ya miamba hao wa Uropa kupoteza mechi ya ligi ya Serie A 4-3 nyumbani mwa Sassuolo kuendeleza musimu mbaya zaidi katika historia ya hivi punde ya klabu hicho.
Mabao yote ya Sassuolo yalipatikana kupitia chipukizi Domenico Berardi, 19, katika tukio lililofanya Allegri kushambuliwa vikali na naibu wa rais wa AC Milan, Barbara Berlusconi.www.skychami.bogsport.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget