http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Nasri kukaa nje miezi miwili





Staa wa Ufaransa na Manchester City, Samir Nasri, anatarajiwa kubaki nje kwa miezi miwili baada ya kujeruhiwa vibaya kwenye goti wikendi iliyopita.


Nasri alipata jeraha lake akichezea City ugenini Newcastle ambapo wlifanikiwa kuwanyamazisha wapinzani wao 2-0 baada ya kuchezewa makosa naye kiungo Mapou Yanga-Mbiwa.
“Asanteni nyote kwa maneno ya kuinua moyo na kuniunga mkono kwa dhati. Habari njema nimepokea ni kuwa natazamiwa kuwa nje kadri ya wiki nane,” Nasri aliandika kwenye anwani yake ya mtandao wa Twitter.

Meneja wa City, Manuel Pellegrini alidokezea wanahabari kuwa Nasri aliumiza mshipa wa goti lake na aligadhabishwa na kuwa Yanga-Mbiwa aliruhusiwa kuendelea na mchezo.www.skychami.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget