http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

United watafuta wokovu wa Capital One


Mabingwa wa Ligi ya Premier ya Uingereza wanaojikwaa, Manchester United, watageukia kombe la Capital One kuokolea musimu wa kutoka ahera watakapotembelea Sunderland Jumanne.
Magwiji hao wamejipata alama 11 nyuma ya viongozi wa Premier, Arsenal, na wikendi iliyopita, walitoswa nje ya Kombe la FA na Swansea waliowanyoa 2-1 ndani ya kasri yao, Old Trafford, kuongezea machungu.
Ingawa United bado wanawania Ligi ya Mabingwa wa Uropa, kombe la Capital One linawakilisha matumaini yao makubwa kunusuru musimu ambao unakondolea kuwa janga kuu.
Motisha zaidi ni kuwa kuna uwezekano mkuu kuwa watawania fainali ya shindano hilo dhidi ya waasimu wao wa jadi na majirani Manchester City ambao wataalika West Ham United katika mkondo wa kwanza wa semi-fainali yao Jumatano.

Meneja wa United, David Moyes, amewania fainali moja pekee wakati alipoongoza Everton kushindania Kombe la FA dhidi ya Chelsea mwaka wa 2009 lakini vijana wake walisalimu amri 2-0.
Huku uga wa Wembley ukinukia, Moyes ameshawishi viungo wake wa sasa wajikakamue ili wasiweze kukumbwa na aibu ya kushindwa tena kwa mshtuko.
“Kupoteza mechi katika klabu chochote ni ngumu. Hapa Manchester United, ni ngumu zaidi,” Moyes alisema baada ya Wilfried Bony kuzamisha timu yake na bao la dakika 90 Jumamosi.
“Hiyo ndio hali ya kazi hii na tutainuka kutoka hapa. Tuna mecbi kubwa Jumanne na tutatayarisha kikosi.”
Sunderland wanavuta mkia wa Premier lakini wameonyesha ishara za ubora kwani wameshindwa mechi moja pekee kati ya tano za mwishowww.skychami.blogspot.com.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget