http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Walcott hatihati ya kutokucheza kombe la dunia hatocheza miezi sita


Theo Walcott 
Arsenal na Uingereza zimepata pigo kuu baada ya mshambuliaji nyota, Theo Walcott, kusemekana hatocheza kadri ya miezi sita baada ya kujeruhi mishipa ya goti, klabu chake kimedhibitisha.
Walcott alipata jeraha hilo dakika za mwisho za mechi yao dhidi ya watanshari Tottenham Hotspurs kwenye kombe la FA Jumamosi, ambayo Arsenal ilitamba 2-0 baada ya kugongana na Danny Rose.

Staa huyo wa miaka 24, hakuonekana kuwa na machungu alipokuwa akitolewa uwanjani na machela pale alipowakejeli mashabiki wa Spurs na kuwakumbusha idadi ya mabao.
“Theo atafanyiwa upasuaji hivi karibuni jijini London na anatarajiwa kubaki nje kwa kipindi cha angalau miezi sita. Kwa hivyo, atakosa musimu uliobaki na Kombe la Dunia la Brazil,” Arsenal walisema kwenye tovuti lao.

Walcott ambaye amechezea taifa lake mara 36, alikosa miezi miwili awali musimu huu na jeraha la matumbo na amedhihirisha umaahiri mkubwa baada ya kurejea.
Amefunga magoli matano katika mechi sawia kabla ya kivumbi cha Jumamosi.
Nyota huyo hataadhibiwa kwa ishara yake iliyodhamiria kuwakera mashibiki wa Spurs lakini kuumia kwake ni pigo kuu kwa matumaini ya klabu na taifa lake.
“Kila mtu Arsenal anamtakia Theo afueni ya haraka na tunatazamia kumkaribisha tena uwanjani haraka iwezakanavyo,” Arsenal waliongezawww.skychami.blogspot.com.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget