http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Magoli mawili ya Ronaldo yainua Real madrid


Cristiano Ronaldo 
Kwa mara nyingine tena, nyota matata, Cristiano Ronaldo, aliibuka shujaa pale mabao yake mawili ya dakika za lala salama yaliposaidia Real Madrid kuchakaza Celta Vigo 3-0 kwenye ligi ya La Liga ya Uhispania.
Kufuatia matokeo hayo, Real walipunguza mwanya baina yao na viongozi Barcelona na Atletico Madrid hadi alama tano baada ya wawili hao kufungua mwaka na ushindani wikendi iliopita.
Huku Madrid wakiwa na shinikizo la kushinda ili matumaini yao ya kunyakua taji yasididimie, Ronaldo na wenzake walijipata wamedhibitiwa vikali na Celta ambao walipoteza nafasi wazi za kufunga kabla ya mshambuliaji wao Karim Benzema kuwapatia uongozi kati kati ya kipindi cha pili.
Ronaldo alikamilisha udhia katika dakika za 82 na muda mchache baadaye, alisherehekea lake la 400 binafsi pale alipounganisha krosi ya Gareth Bale na kutia kibindoni.

“Hilo halikuwa onyesho nzuri na tunafaa kukaza kamba katika ngome,” kocha wa Real, Carlo Ancelotti, aliambia wanahabari.
“Tulikosa mwelekeo na wachezaji wengi wetu walikimbia mbele na kuwacha nyuma wazi jambo ambalo lilialika mashambulizi.”
Barcelona na Atletico Madrid wamezoa alama 49 baada ya kubwaga Elche na Malaga.www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget