http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Torres kukaa nje wiki kadhaa kutokana na jeraha


Fernando Torres 


Fernando Torres atakaa “wiki kadha” bila kucheza baada ya kupata jeraha la kano ya goti wakati wa ushindi wa 3-1 wa Chelsea dhidi ya Manchester United Jumapili, meneja Mourinho amesema.
Torres aliingia kama nguvu mpya mechi ikikaribia kumalizika kumpumzisha straika wa Cameroon Samuel Eto'o, ambaye mabao yake mawili yalihakikisha Chelsea wanaendelea kupigania taji la Ligi ya Premia.

"Tutakuwa bila Fernando Torres kwa wiki kadha kutokana na kano zake za goti,” Mourinho aliambia wanahabari.
Aliongeza kuwa straika wa Senegal Demba Ba sasa atachezeshwa licha ya kutochezea Chelsea tangu kichapo walichopokezwa League Cup na Sunderland Desemba 17.
"Wakati wa Demba umefika. Ni jambo la kusikitisha kwa sababu Torres amekuwa katika hali nzuri kwa sasa,” Mourinho alisema.
"Demba alikuwa na wiki nzuri, ilikuwa vigumu sana kwangu kumuacha nje ya timu kwa sababu alitia bidii sana, sana.
"Mechi zijazo sasa ni za Demba au Samuel."www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget