http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Moyes akiri ana 'kibarua kigumu'


David Moyes 




Meneja wa Manchester United David Moyes amekiri kwamba anakabiliwa na “kibarua kigumu” baada ya mabingwa hao kushindwa 3-1 ugenini kwa Chelsea katika Ligi ya Premia Jumapili.
Mashabiki wa Chelsea waliimba muda wote wa mechi wakitaka Moyes abaki kwenye kazi yake, na kumuongezea presha raia huyo wa Scotland ambaye timu yake imejipata alama 14 nyuma ya viongozi Arsenal huku meneja huyo akijaribu kutoshea kwenye viatu vikubwa vya mtangulizi wake Alex Ferguson.
"Ni kibarua kigumu. Nilikuwa nimetumai tutakuwa katika nafasi nzuri kuliko ilivyo sasa lakini hilo halijakuwa,” Moyes aliambia wanahabari.
"Kwa hivyo nina kibarua kigumu. Lakini nafikiri ukiwa mtu wa soka, ni kibarua chema kuwa nacho. Nasubiri kwa hamu kukikabili.”

Ingawa United wako alama14 nyuma ya viongozi Arsenal baada ya mechi 22, Moyes alikataa kufutilia mbali matumaini ya kutetea taji.
“Kile ambacho huwa hatufanyi ni kufa moyo hadi tufike hapo. Kazi ni kujaribu na kumaliza wa kwanza,” akasema, na kuweka kando madai kwamba United wanakabiliwa na mzozo wakiwa nambari saba kwenye ligi.
"Hakuna majibu ila tu kujaribu na kushinda mechi inayofuata,” akasema.
Moyes alieleza kusikitishwa kwake na kushindwa kufunga kwa timu yake baada ya wachezaji wake kupoteza nafasi nyingi za kufunga mapema na pia kukosa kujilinda vyema na kupelekea straika wa Chelsea Samuel Eto'o kufunga mabao matatu.
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho alimuonea huruma Moyes, akisema United ndio waliokuwa wazuri mechi hiyo.
"Ni vigumu sana kwao kucheza vyema hivyo dakika 20 au 25 za kwanza na kisha washindwe,” Mreno huyo alisema.
Lakini Mourinho alisema anafikiri kwamba United kwa sasa wako nyuma sana ya timu tatu zinazoongoza ligi kiasi kwamba hawawezi kuzifikia.
"Sidhani David atakasirishwa name nikimwambia ukweli, ambao ni kuwa kuna mwanya wa alama 14 (kati yao na Arsenal) na 13 na 12 (na Manchester City na Chelsea). Wanaweza kujikwamua na kufikia moja ya timu hizi? Wanaweza,” akasema.
“Lakini kujikwamua na kufikia timu hizo zote tatu, itahitaji tatu kuwa ni kama zimesambaratika. Nadhani kuhusu taji, itakuwa vigumu kwao.”www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget