http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Messi afaa Barca kwa mabao mawili


Leo Messi 




Nyota Lionel Messi alifunga mabao mawili na kusaidia Barcelona kulaza Getafe 2-0 na kufuzu kwa jumla ya mabao 6-0 kwa robofainali ya King's Cup lakini wakampoteza Neymar kutokana na jeraha katikati ya kipindi cha kwanza.
Messi na Neymar walikuwa wamerudi kwenye kikosi cha kwanza lakini fowadi huyo wa Brazil alikaa tu dakika 25 uwanjani baada ya kupinda tindi yake ya mguu na akaondolewa kwa machela.
Ilikuwa ni mara yake kwa nahodha wa Argentina Messi kuanza kwenye mechi tangu apate jeraha la misuli ya paja Novemba iliyopita na alionekana hatari sana mbele ya goli.
Baada ya kufunga la kwanza karibu na muda wa mapumziko, alifanya mambo tena baada ya mapumziko alipokimbia kama kawaida yake na kupiga chenga wachezaji kadha na kisha akambwaga kipa Jordi Codina aliyekuwa amepiga mbizi na akautuma mpira wavuni
.
Xavi aliingia kama nguvu mpya kipindi cha pili na kuchezea Barcelona mechi yake ya 700.
Real Sociedad pia walisonga mbele kwa ushindi wa 1-0 wakiwa Villarreal, kwani walikuwa wametoka sare ya 0-0 kwenye mechi yao ya mkumbo wa kwanza katika16 bora.www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget