http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Shabiki mlevi apiga 999 kudai Ferguson




Polisi wa Uingereza wametibua kwamba shabiki aliyelewa wa Manchester United alipiga simu kwenye namba ya dharura ya 999 akitaka kuzungumza na meneja aliyestaafu, Sir Alex Ferguson, baafa ya timu hiyo kubanduliwa kombe la League Cup.
Mfuasi huyo aliyejawa na gadhabu aliwashangaza walinda sheria pale alipopiga 999 dakika chache baada ya United kuanguka mikononi mwa Sunderland baada ya penalti katika semi-fainali ya shindano hilo Jumatano.
Simu hiyo ilipokewa majira ya saa 10:30 usiku saa za Uingereza kutoka mwanaumme aliyepiga kutoka Crumpsall, Manchester kaskazini na kulingana na kikosi cha Greater Manchster Police, jamaa huyo alikuwa amekerwa sana.
“Shabiki huyo alipiga simu akiwa kwenye hali ya kulewa kupindukia akitaka kuzungumza na Sir Alex Ferguson.
“Ingawa ni jambo la kuhuzunisha kwa kila shabiki wakati timu yake inapopoteza mechi, ni muhimu kufahamu 999 inatumika kwa dharura pekee.
“Ikiwa unataka kuongea na Ferguson kuhusiana na matokeo ya majuzi, sisi hapa GMP tungeomba ujaribu kupigia Manchester United FC wenyewe kwani una nafasi njema ya kumpata badala ya kupigia polisi,” taarifa ya polisi ilisema.
Fedheha ya Jumatano iliongezea United masaibu katika musimu wao wa kwanza tangu Ferguson astaafu Mei iliyopita.www.skychami.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget