http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Chelsea wamsainisha Sala



mohamed salah
Chelsea wamesonga kuziba pengo litakalowachwa na kuwauzia Manchester United Juan Mata kwa kumsajili Mohamed Salah kutoka klabu cha Uswisi, Basel.
“Hii itategemea na mchezaji huyo wa kitaifa wa Misri kukubaliana matakwa yake binafsi na kukamilisha mtihani wa kimatibabu,” klabu hicho kilisema kwenye tovuti lao.
“Kiungo huyo alifunga dhidi yetu mara mbili katika Champions League mapema musimu huu na alishamiri kwenye semifainali ya kombe la Europa mwaka jana.
Kitita cha kumleta Salah Chelsea hakijulikani rasmi lakini taarifa Uingereza zinasema anaweza kugharimu kiasi cha pauni milioni 16 za milki hiyo.
Mchezaji huyo, 21, atakalia nafasi tatu zilizotengewa kitengo chake nyuma ya mshambuliaji wa pekee kwenye muundo wa 4-2-3-1 unaotumika na meneja Jose Mourinho.www.skychami.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget