| |
Watford, ambao walishindwa kwenye mechi ya marudiano ya fainali katika Championship msimu uliopita, walienda mbele 2-0 katika dakika 30 za kwanza kupitia Fernando Forestieri na Troy Deeney na kuacha City ambao wamekuwa wakifunga mabao kadiri wanavyopenda wakikodolea macho kichapo cha kushangaza.
Hata hivyo, Aguero alifunga mara tatu nusu saa ya mwisho, huku pia Aleksandar Kolarov naye pia akifunga, na kupelekea City ambao msimu uliopita walishindwa kwenye fainali kufuzu kwa raundi ya tano.
Kutokana na hali kwamba Watford wamo nambari 15 katika Championship, hawakuwa wakitarajiwa hata kidogo kushangaza wenyeji Etihad Stadium, lakini walifunga la kwanza dakika ya 21pale Forestieri alipombwaga Costel Pantilimon.
Ilikuwa ni zawadi kwa wageni hao kutokana na ujasiri walioanza nao mchezo na dakika tisa baadaye walifanya mambo kuwa 2-0, baada ya Deeney kukamilisha uchezaji mzuri ambao ulishirikisha pia Sean Murray na Ikechi Anya.
Meneja wa City Manuel Pellegrini aliwaingiza madifenda Vincent Kompany na Pablo Zabaleta kipindi cha pili na huku kukiwa kumesalia nusu saa ya mchezo, wenyeji walikomboa bao moja kupitia Aguero.
Mwargentina huyo alikamilisha krosi safi kutoka kwa Kolarov na dakika ya 79 pia alifunga la kusawazisha, kwa kupenyeza mpira kwa kutumia guu lake la kushoto na kufunga bao lake la 24 msimu huu.
Watford bado walikuwa na matumaini ya kujiwekea mechi ya marudiano, lakini zikiwa zimesalia dakika tatu pekee Kolarov akamhadaa kipa mgeni Jonathan Bond kutoka hatua 40 na kufanya mambo 3-2 kabla ya Aguero kukamilisha matatu yake dakika ya mwisho.
Liverpool pia walikwepa kichapo kwa kushinda 2-0 ugenini kwa timu ya daraja la pili Bournemouth.
Kwenye mechi hiyo iliyochezewa uwanja ulioangaza jua katika pwani ya kusini Uingereza, Liverpool walihimili mashambulizi makali ya mapema kutoka kwa wenyeji kabla ya kujiweka kifua mbele dakika ya 26 kupitia Victor Moses.
Daniel Sturridge alifanya mambo kuwa 2-0 kukiwa na nusu saa ya kucheza iliyosalia, baada ya kufikia pasi safi kutoka wka Suarez na kumbwaga kipa Lee Camp mbele ya macho ya meneja wa Uingereza Roy Hodgson.
Meneja wa Liverpool Brendan Rodgers alimsifu mpinzani wake Eddie Howe kwa vile Bournemouth walivyocheza.
"Unapokuwa na timu ambayo inataka kucheza soka, hao ndio wachezaji wajasiri zaidi uwanjani,” akasema.
“Ni rahisi sana kwa kocha wa timu kuketi kitako, kutotaka kuwa na mpira na kujilinda pekee, na kisha kusubiri nafasi tu ya kufunga. Bournemouth ni timu nzuri na nawasifu sana mbele ya yote. Eddie anafanana name katika filosofia yake ya soka.”www.skychami.blogspot.com
Post a Comment