| |
Suarez amefunga mabao 22 katika mechi 16 za ligi ya Premier ya Uingereza tangu arejee Septemba baada ya kutumikia adhabu ya mechi 10 kutokana na makosa ya kuuma mlinda ngome wa Chelsea, Branislav Ivanovic, kwenye mechi yao Anfield Aprili iliyopita.
Straika huyo wa Uruguay amewashinikiza wanahabari wa Uingereza kumtaja kama miongoni mwa wachezaji bora zaidi duniani kimo cha Lionel Messi na Cristiano Ronaldo aliyetunukiwa taji la Ballon d’ Or Jumatatu.
“Unatilia mashabiki bidii na ni muhimu miezi kadhaa iliyopita imeguwa migumu kwangu. Sasa, nimebadilika na kila kitu ki sawa.
“Hilo linaathiri Liverpool pia kwani hatujacheza vyema misimu miwili au mitatu iliyopita na sasa tumerejelea hali mzuri,” Suarez aliambia tovuti la klabu chake www.liverpoolfc.com , Jumanne.
Suarez alifunga mawili dhidi ya Stoke City Jumapili katika ushindi wa Liverpool wa 5-3 ugenini.
Ilikuwa mara yake ya nane musimu huu kufunga mawili au zaidi.www.blogspot.com
Post a Comment