http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Wilshere amerejea na kiwango bora zaidi- Wenger


Jack Wilshere 
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ametangaza kuwa kiungo wake Jack Wilshere, anafikia kimo cha ubora wake wakati ambao musimu wa ligi ya Premier unazidi kuchacha.
Kiungo huyo raia wa Uingereza aliibuka shujaa katika ushindi wao wa 2-1 dhidi ya Aston Villa, Jumatatu usiku, uliorejesha Arsenal kileleni cha Premier.
Wilshere alipata goli la kwanza kabla ya kubuni la pili lililozamishwa wavuni na Mfaransa Olivier Giroud huko onyesho lake likichangamsha matumaini ya Arsenal na taifa lake Uingereza kubobea katika Premier na Kombe la Dunia kwa mpangilio huo
.
“Amepata kasi kwenye mchezo wake na pia kina kwani yeye si mwadili wa pasi pekee yake lakini ni jamaa anayeweza kubuni akiwa na mpira,” Wenger aliambia wanahabari.
“Ubora wake unahitaji awe katika hali bora zaidi ya mchezo,” aliongeza.
Ingawa Wilshere alianza kampeni yake ya sasa kwa ulegevu, kiungo huyo amezidi kuwa mwamba wa harakati za Arsenal kutwaa ubingwa wa Premier huku bao lake likiwa la kwanza tangu Oktoba.
“Mara nyingine, ninalazimika kucheza maeneo wazi na wakati mwingine, natumika kati lakini bora timu inafanya vyema na kupata alama tatu ndio muhimu,” Wilshere alinena.www.skychami.blospot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget