http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Cardiff wamchukua Fabio, Jones, wakaribia kumnasa Zaha


Fabio da Silva




Cardiff City wamechukua beki wa kushoto wa Manchester United na raia wa Brazil Fabio na pia straika wa Stoke City Kenwyne Jones, meneja wa klabu hiyo ya Ligi ya Premia Ole Gunnar Solskjaer alisema Jumatatu.
Cardiff pia wanatarajia kumpata winga wa Manchester United Wilfried Zaha kwa mkopo kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kuhama wachezaji Ijumaa.
"Fabio na Kenwyne watajiunga nasi kwenye mazoezi leo. Nimekutana nao tu saa hizi na ni kama kila kitu kimekamilishwa,” Solskjaer aliambia kikao cha wanahabari Manchester kabla ya mechi yao ya Ligi Kuu ya Uingereza dhidi ya United Jumanne.
Solskjaer, ambaye ni raia wa Norway, na aliyechukua hatamu Cardiff mwezi huu, alisema mktaba wa Zaha bado haujakamilishwa.
“Tunatarajia kukamilisha hilo katika saa 24 hivi, ili awe tayari kwa wikendi,” straika huyo wa zamani wa Manchester United alisema.
Cardiff wameshuka hadi mwisho wa jedwali na wamo hatarini ya kushushwa ngazi msimu mmoja tu baada yao kupanda ngazi kucheza Ligi ya Premia kwa mara ya kwanza kabisa mwaka jana.www.skychami.blogsports.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget