http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Mourinho asema hatumii tena hela Januari


Jose Mourinho 






Jose Mourinho amefichua kwamba Chelsea hawapangi kununua wachezaji wengine kabla ya kipindi cha sasa cha kuhama wachezaji kumalizika.
Mdosi huyo wa Blues tayari amenasa Nemanja Matic na Bertrand Traore, huku winga wa Misri Mohamed Salah akitarajiwa kukamilisha kuhama kwake kutoka kwa klabu ya Basle ya Uswizi atakapopita uchunguzi wake wa kimatibabu na kuafikiana na klabu kuhusu matakwa yake ya kibinafsi.
Traore, 18, tayari amekabidhiwa Vitesse Arnhem kwa mkopo, lakini Salah na Matic, aliyerudi Stamford Bridge kwa ada ya £21 milioni baada ya kukaa Benfica, wote wawili wanatarajiwa kuanza kuchezea klabu hiyo mara moja.
Mpango wa awali wa Chelsea mwezi huu ulikuwa wa kumwendea Matic pekee, lakini kuuzwa kwa Juan Mata kwa Manchester United na Kevin De Bruyne aliyehamia klabu ya Bundesliga ya Wolfsburg kulimshawishi Mourinho kumnunua Salah aliye wa thamani ya £10 milioni.
Na huku kipindi cha kununua wachezaji kikimalizika Januari 31, Mourinho anaamini huo ndio mwisho wa Chelsea wa kusaka wachezaji.

"Natumai tumemaliza,” Mourinho alisema. “Hatununui straika wakati huu.”
Hiki ni kipindi cha mpito kwa Chelsea ukiwa ni msimu wa kwanza baada ya Mourinho kurudi London magharibi, lakini bado wanapigania Ligi ya Premia na watakutana na Galatasaray katika 16 Bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Mourinho, ambaye macho yake wikendi hii yanaangazia mechi ya raundi ya nne ya Kombe la FA dhidi ya Stoke Jumapili alisema: “Tungenunua tu Nemanja wakati huu kama hatungempoteza mchezaji (Mata), lakini tunajaribu kudumisha kiwango na kuimarisha kikosi ili kubadilisha mtindo wa kucheza.
“Na bado tunajaribu kupata matokeo mema na kushinda mechi. “Tunahitaji mchanganyiko huo wa wachezaji chipukizi wanaokomaa na wale waliokomaa na wenye uzoefu ili kuipa timu uthabiti.
“Tunafanya hivyo. Mnaweza kuona yale tunajaribu kufanya. Nemanja (Matic) ana miaka 26, Salah 21, na kwa hivyo tunajaribu kujenga timu ya siku za usoni.”www.skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget