Difenda wa Everton Leighton Baines amerefusha muda wake wa kukaa katika klabu hiyo baada ya kutia saini mkataba mpya wa miaka minne, klabu hiyo ya Ligi ya Premia ilitangaza Jumatatu.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alikuwa amesalia na miezi 17 kwenye mkataba wake Goodison Park na licha ya ripoti kwamba alikuwa akitafutwa na meneja wake wa zamani David Moyes akajiunge naye Manchester United, beki huyo wa kushoto wa umri wa miaka 29 aliambia kusalia Goodison Park.
"Hatuwezi kueleza furaha tuliyo nayo kwamba klabu hii imepata miaka bora ya uchezaji wa Leighton Baines," meneja Roberto Martinez aliambia tovuti rasmi ya klabu hiyo (www.evertonfc.com).
"Ni jambo la kutuongeza nguvu sana na la kuleta msisimko kuhusu siku za usoni. Leighton ametimiza tu miaka 29 majuzi na ana kiwango cha ukomavu na ujuzi wa soka katika pahala maalum uwanjani, na kuwepo kwake kwenye kikosi husikika.”
Baines alijiunga na Everton kutoka Wigan mwaka 2007 na amekuwa na kuwa mmoja wa wachezaji wanaotegemewa sana na klabu hiyo ambayo ameichezea zaidi ya mara 260.
Pia ni mwanachama muhimu wa kikosi cha Uingereza chini ya Roy Hodgson na anapigania nafasi ya kuwa wa kwanza kwenye mechi na Ashley Cole wa Chelsea taifa hilo likijiandaa kwa Kombe la Dunia nchini Brazil mwezi Juni.
"Ninajua kwamba kila shabiki atakuwa na furaha kutokana na habari hizi na tuko pamoja katika msisimko huu tukiangalia sehemu iliyosalia ya msimu huu na hata baadake,” Martinez akaongeza.
"Kutokana na mechi muhimu zilizo mbele yetu, itakuwa muhimu sana kuwa na uzoefu wa Leighton kutuwezesha kupigania malengo yetu.”
Everton walianza vyema msimu chini ya Martinez tangu Mhispania huyo achukue pahala pa Moyes mwanzoni mwa msimu na kwa sasa wako nambari sita kwenye Ligi ya Premia, alama moja pekee nyuma ya jirani zao Merseyside Liverpool, ambao wako nambari nne.
Klabu hiyo pia imefuzu kwa raundi ya tano ya Kombe la FA ambapo wameratibiwa kucheza nyumbani dhidi ya Swansea City.www.skychami.blogspot.com
Post a Comment