http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

MESSI'BALOTEL OZIL NI MIONGONI MWA MASTAA WANAONGOZA KWA KUVUTA SIGARA WENGER AMCHIMBA MKWARA WILSHERE

kiungo wa arsenal jack wilshere wakivuta sigara na mke wake
BOSI wa Arsenal Arsene Wenger amemuonya Kiungo wake Jack Wilshere hadharani baada kupigwa picha akivuta nje ya Naiti Klabu moja huko London.
Wilshere alipigwa picha akiwa na Sigara mkononi nje ya Klabu ya Usiku Jijini London Usiku wa baada ya Mechi ambayo Arsenal iliifunga Napoli 2-0 kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amechukua hatua ya nadra ya kumuonya Mchezaji huyo hadharani.
Wenger alisema: “Sikubaliani kabisa na tabii hii! Nahitaji kuzungumza nae kuhusu hilo. Ukiwa Mchezaji Soka wewe ni mfano na hufanyi vitu vya kuumiza afya yako…hii pia inaweza kuharibu sifa yako.”
Wenger aliongeza: “Siku hizi vitu ni tofauti. Nimesafiri kwenye Basi kama Mchezaji huko France na ndani ilikuwa hamuonani kwa moshi wa Sigara. Lakini sasa mambo yamebadilika na Wachezaji Soka ni mifano ya kuigwa…!”
Hata hivyo, Wenger alikataa kuzungumza nini hasa ataongea na Wilshere na adhabu gani ya utovu wa nidhamu atapewa na badala yake alisisitiza kuwa Kiungo huyo mweye Miaka 21 ni mmoja wa Wachezaji muhimu wa Kikosi chake.
Alisema: “Ni Mchezaji muhimu hapa. Plani zangu za baadae pia zimhusisha Wilshere.”Hawa ndo kumi bora
 
1 Jack Wilshere
2 Lionel Messi
3 Zinedine Zidane
4 Mario Balotelli
5 Laurent koscielny
6 Dimitar barbatov
7 Diego Maradona
8 Mesut 0zil
9 Wayne Rooney
10 Socrate

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget