jana Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam uligeuka vurugu tupu mara baada ya Kagera Sugar kusawazisha Bao kwa Penati katika Dakika za Majeruhi na Mashabiki kung’oa Viti na kuvitupa Uwanjani hali ambayo iliwalazimu Polisi kufyatua Mabomu ya Machozi.
Mechi hiyo ilimalizika kwa Bao 1-1 na kuiacha Simba ikibaki Nafasi ya 4 huku Kagera Sugar ikipanda nafasi moja.
Simba ndio waliotangulia kupata Bao katika Dakika ya 45 ambalo llifungwa na Mchezaji toka Burundi, Amisi Tambwe, alieinasa pasi ya Betram Mombeki na kuwatambuka Mabeki Salum Kanoni na Ernest Mwalupani na kisha kufunga.
Huku Simba wakitegemea ushindi kwani Bango la Dakika za Nyongeza lilikuwa limeshaanikwa na Refa wa Akiba likionyesha Dakika 4 na nusu ya Dakika hizo kuyoyoma, Beki wa Simba Joseph Owino akamwangusha Daudi Jumanne ndani ya Boksi na Refa kutoa Penati iliyofungwa na Salum Kanoni.
Alhamisi Jioni kwenye Uwanja wa Taifa JKT Ruvu watapambana na Mabingwa Watetezi Yanga kwenye Mechi pekee ya Ligi Kuu Vodacom ambapo ushindi kwa Yanga utawafanya wakamate usukani wa Ligi.
Post a Comment