http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

Exclusive: Jokate ameyaongea yote kuhusu mapenzi yake na Hasheem Thabeet na Diamond hapa

Jokate 123So baada ya kuona headline kwenye Jarida la VibeTz ambalo liko mitaani kuanzia leo October 18 2013 kuhusu Jokate kuzungumzia kwa mara ya kwanza uhusiano wake wa kimapenzi na mwimbaji Diamond Platnumz na mcheza kikapu Hasheem Thabeet, J amekubali pia kuzungumza na millardayo.com na kuweka wazi baadhi tu ya vitu vichache kati ya vingi alivyoongea na VibeTZ.
Yafuatayo ni maswali machache ya Millard Ayo kwa Jokate:
Millard Ayo: Nini kimekufanya ufunguke na hizi info ambazo hujawahi kuzizungumzia na mara nyingi umekua ukigoma kuziongelea kwenye media?
Jokate: Nahisi kwa sababu watu wanazidi kuizungumzia na wanaizungumzia sivyo, hawazungumzii kiuhalisia na kiukweli inanisumbua ndio maana nimeamua kusema kitu kidogo alafu niufunge huu ukurasa.
Millard Ayo: Imekua ikikusumbua kwa mda gani?
Jokate: Kwa muda mrefu, toka mwaka jana… kwenye facebook watu wanatoa comment na najua kabisa watu hawajaelewa hili swala na mimi sipendi mashabiki wangu kutokunielewa.
2 kamili
 millard umewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Diamond pamoja na Hasheem?
Jokate: Hahahahahhaha !!!! Yeah..
Millard Ayo: Uhusiano wa nani kati ya hawa wawili ulidumu kwa muda mrefu?
Jokate: Wa Hasheem.. karibia miaka miwili mitatu
Millard Ayo: Na wa Diamond?
Jokate: Oooh kipindi kifupi sanaaa, sijui mwezi sijui miezi miwili… kidogo alinipa tabu, ila kiukweli nilitaka tu kwa sababu kuna watu wengi walikua wanasema Jokate yani vurugu, unajua sio kila kitu unachokisikia ndio chenyewe na media saa nyingine inapenda kuandika vitu ambavyo sio vya ukweli au wanaviwasilisha sivyo.
Jokate na Diamond
Millard Ayo: Sasa hivi uko single?
Jokate: Yeah, kwa muda mrefu tu niko mwenyewe alafu saa nyingine wananisumbua lakini nafurahia kwa sababu naweza kufocus kwenye kazi zangu mfano wiki ijayo nakwenda kushoot movie na JB, muziki na biashara zangu kwa hiyo inanipa fursa nzuri kufanya vitu vyangu, yani mwenyewe kujiamulia asubuhi nakwenda kufanya vitu vyangu hivyo bila kusumbuliwa si unajua Wanaume wanaweza kusema wanataka attention nini… sio kitu kibaya atleast kwa sasa hivi.
Millard Ayo: Umekaa single kwa muda gani sasa hivi? zaidi ya mwaka?
Jokate: Yeah, kwa zaidi ya mwaka mmoja… sijawa na mtu ambae nimeweza kumuita like oohh this is my boyfriend… najua ni ngumu lakini nabusubusu watu wengi…. hahah a hah natania hapo, basi tu imetokea hivyo pengine bado sijapata mtu ambae nimeona ataweza kuwa kama wale..
Jokate, Hasheem na Ally.
Jokate, Hasheem na Ally.
Unaweza kujiunga na kuwa mwanafamilia wa millardayo.com ili kupata info zote zinazotufikia za siasa, michezo, muziki, maisha, movie na nyingine kwenye @millardayo facebook, twitter na instagram kwa jina hilohilo.
Usisahau kuchukua kopi ya jarida la VIBE ambalo lipo mtaani kuanzia leo ili uone jinsi Jokate alivyofunguka vya kutosha humo ndani..
Hapa chini unaweza kusikiliza interview yote ya Jokte aliyofanyiwa na Millad source millard ayo

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget