http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

CITY YAMALIZA REKODI YA KUTOFUNGWA EVERTON

!Kipigo cha Everton Uwanjani Etihad mikononi mwa Wenyeji Manchester City cha Bao 3-1, kimefuta rekodi ya Everton ya kuwa Timu pekee ambayo ilikuwa haijafungwa kwenye Ligi Kuu England Msimu huu. Everton ndio walitangulia kufunga kwa Bao la Mchezaji wa Mkopo kutoka Chelsea, Romelu Lukaku na kudumu Dakika moja tu kwa City kusawazisha kwa Bao la Dakika ya 17 kuvitia Alvaro Negredo na Sergio Aguero kuipa City Bao la Pili kabla Haftaimu. Bao la tatu la City lilifungwa kufuatia Penati ya kilaini iliyotolewa baada Zabaleta kusukumwa huku Everton wakinyimwa Penati ya aina hiyo hiyo kufuatia kuangushwa Lukaku. Aguero alipiga Penati hiyo iliyochezwa na Kipa Tim Howard na kugonga mwamba na Mpira kumbabatiza Kipa huyo na kutinga. Ushindi huu umewafanya Man City wapande hadi Nafasi ya Pili wakiwa wamecheza Mechi moja zaidi na hivyo Mechi za baadae zinaweza kuwang’oa Nafasi hiyo. VIKOSI: MAN CITY: Hart, Zabaleta, Kolarov, Kompany, Lescott, Milner, Fernandinho, Toure, Silva, Aguero, Negredo Akiba: Richards, Nasri, Dzeko, Jesus Navas, Clichy, Pantilimon, Nastasic. EVERTON: Howard, Baines, Distin, Jagielka, Coleman, McCarthy, Osman, Naismith, Barkley, Mirallas, Lukaku Akiba: Robles, Gibson, Heitinga, Jelavic, Kone, Deulofeu, Stones. Motokeo mengine haya hapa lakini bado michezo inaendelea Cardiff City 0 - 2 Newcastle United HT Fulham 0 - 0 Stoke City HT Hull City 0 - 0 Aston Villa HT Liverpool 3 - 0 Crystal Palace magoli ya liverpool yakiwekwa kimiani na Suárez dakika ya 13 D. Sturridge dk ya 17 na gerrald dk ya 38 newcastle nao wanaongoza kwa goli mbili bila

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget