http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

CARDIFF CITY! WADAI BAO LA CHELSEA, SI HAKI

CHELSEA-BAO_LA_MZOZO
WALIKUWA nyuma kwa Bao 1-0, wakiwa kwao Stamford Bridge, na Chelsea kusawazisha Bao ambalo sasa limezua Mjadala mkubwa kwenye anga za Soka.
Meneja wa Cardiff City, Malky Mackay, ambae leo Timu yake imechapwa Bao 4-1 kwenye Mechi ya Ligi Kuu England licha ya kuongoza kwa Bao 1-0, amemlaumu Refa Anthony Taylor kwa kufanya uamuzi uliobadilisha Gemu yao hiyo.
Jordon Mutch alitangulia kuipa Bao Cardiff City lakini Chelsea walijibu katika Dakika ya 33 baada ya Kipa wa Cardiff City, David Marshall, aliekuwa amaedaka Mpira, kuudunda Mpira chini na Samuel Eto’o kuudokoa na baadae kumfikia Hazard aliefunga lakini Wachambuzi wamebainisha kuwa Kisheria Goli hilo lingetakiwa kutokubaliwa.
Ingawa Chelsea waliongeza Bao 3 zaidi baada ya Bao hilo, lakini Meneja Malky Mackay anaamini makosa ya Refa Anthony Taylor kulikubali Bao hilo la kusawazisha ndio limewaua.
Alisema: “Ilitakiwa kuwa ni faulo lakini imewapa Goli na tumekwenda Haftaimu 1-1 badala ya sisi kuwa 1-0 mbele. Ni kosa kubwa!”
Baada ya Mechi Mackay aliiambia Sky Sports: “Nilikwenda kuongea na Refa kutaka kujua nini kimetokea akaruhusu Bao lile. Refa Msaidizi alidhani Kipa aliuweka Mpira chini! Nikamuuliza kama kaudunda je? Akajibu kama aliudunda sio Goli ni faulo lakini sie tulijua kauweka chini!”
Akisikitika, Mackay alizungumza: “Unaweza kutazama picha na kuona waziwazi Mpira !”source soka in bongoulidunda posted by skychami.blogspot.com

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget