http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

BRAZIL YAICHAPA ZAMBIA GOLI MBILI

Chipolopolo walicheza kiume lakini Bao za Dakika ya 59 na 65 za Oscar na Dede ndizo ziliwaua. Brazil walitinga kwenye Mechi hii wakifanya mabadiliko ya Wachezaji 6 kwenye Kikosi chao kilichowafunga South Korea Bao 2-0 huko Seoul hapo Ijumaa na huu ni ushindi wao wa 10 katika Mechi 11 wakiwa wamefungwa Mechi moja tu Mwezi Agosti walipotunguliwa 1-0 na Switzerland kwa Bao la Dani Alves kujifunga mwenyewe. Zambia, ambao hawakufuzu kwenda Brazil kwa Fainali za Kombe la Dunia za Mwakani na wakicheza chini ya Kocha wa muda Patrice Beaumelle baada ya Kocha wao Mfaransa Hervé Renard kuhamia Klabu ya France FC Sochaux, walitinga kwenye Mechi hii bila ya Wachezaji wao watatu muhimu wanaochezea TP Mazembe ya Congo DR. Wachezaji hao wa Chipolopolo, Nathan Sinkala, Stoppila Sunzu na Rainford Kalaba, waliripotiwa na Chama cha Soka Zambia, ZFA, kuwa walichelewa kufika lakini habari toka Zambia zilidai Wachezaji hao wametolewa amri ya kukamatwa na Idara ya Uhamiaji ya Zambia. Inadaiwa TP Mazembe ilikataa kuwaruhusu Wachezaji hao kwa madai wanaumwa Malaria na Tumbo lakini ZFA ikalazimisha waende Zambia kwa uchunguzi na walipofika Zambia Wachezaji hao waliamriwa kusafiri na Timu kwenda China lakini waliyeyuka na kurudi Congo bila kufuata taratibu za Uhamiaji kwa mujibu wa Idara ya Uhamiaji. VIKOSI: BRAZIL: Cavalieri, Dani Alves, Dede, David Luiz, Maxwell, Lucas Leiva, Ramires, Lucas Moura, Paulinho, Pato, Neymar Akiba: Hernanes, Luiz Gustavo, Henrique, Oscar, Dante, Jo, Jefferson, Marcello, Victor, Hulk, Bernard ZAMBIA: Mweenea, Chingo, Chama, Himoonde, Mbola, Lungu, Katongo, Mtonga, Mayuka, Tembo, Mulenga Akiba: Musonda, Chamanga, Kampamba, Kola, Chivuta, Chisenga, Titima, Musakanya

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget