http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

LIGI KUU ENGLAND: WAPYA KUONEKANA JUMAMOSI!

ETOO_IN_CHELSEAMAROUANE_FELLAINI-NEW_IN_MAN_UNITEDOZIL, FELLAINI, ETO’O, WILLIAN, ERIKSEN!!!
MESUT_OZILLIGI KUU ENGLAND inarudi dimbani Jmamosi baada ya kutoonekana kwa Wiki mbili na safari hii shauku kubwa ni kuwaona Wachezaji wapya wakichezea Klabu zao mpya kwa mara ya kwanza tangu wasainiwe kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa hapo Jumatatu Septemba 2.
Jumamosi 14 Septemba
14:45 Manchester United v Crystal Palace
17:00 Aston Villa v Newcastle United
17:00 Fulham v West Bromwich Albion
17:00 Hull City v Cardiff City
17:00 Stoke City v Manchester City
17:00 Sunderland v Arsenal
17:00 Tottenham Hotspur v Norwich City
19:30 Everton v Chelsea

Miongoni mwa hao wapya ni Mesut Ozil, Willian, Marouane Fellaini, SamuelEto’o na Christian Eriksen, ambao huenda ama wakaanza Mechi hizi za Jumamosi.
Mashabiki wa Arsenal wanangoja kwa hamu kumuona Kiungo wa Germany, Mesut Ozil, akivaa Jezi ya Arsenal huko Stadium of Light watakapocheza na Sunderland.
Ozil alihamia Arsenal kutoka Real Madrid kwa Dau la Pauni Milioni 42.4 na kumfanya awe Mchezaji wa Bei ya juu katika Historia ya Arsenal na huko kwao Germany.
Tottenham, baada ya kumpoteza Gareth Bale kwa Real Madrid waliomnunua kwa Dau kubwa Duniani la Pauni milioni 86, wanaweza kumpa Jezi kwa mara ya kwanza Christian Eriksen kutoka Denmark.
Mabingwa Watetezi Manchester United, ambao wako nyumbani kucheza na Crystal Palace katika Mechi ya kwanza kabisa ya Wikiendi hii, huenda wakamchezesha Marouane Fellaini kwa mara ya kwanza.
Nao Chelsea wanaweza wakawacheszeha wapya wao wawili waliowanunua kutoka Klabu ya Urusi Anzhi Makhachkala, Mchezaji kutoka Brazil Willian na Samuel Eto’o wa Cameroun, kwenye Mechi yao ya Ugenini huko Goodison Park watakapocheza na Everton.
Wengine wapya ambao wanaweza kuonekana kwa mara ya kwanza ni Libor Kozak wa Aston Villa, Victor Anichebe akiichezea West Brom na Peter Odemwingie akivaa Jezi ya Cardiff City.
Jumatatu Usiku, Vinara wa Ligi, Liverpool ambao wako Ugenini huko Liberty Stadium kucheza na Swansea City, nao huenda wakawapa Namba wapya wao kwa mara ya kwanza Wachezaji Mamadou Sakho na Tiago Ilori.

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget