http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

BAADA YA STARS KUFUNGWA SASA NI ZAMU YA LIGI KUU TANZANIA BARA


VPL_2013-14_LOGO-NEWBAADA ya Wiki mbili za ‘Vakesheni’ kuipisha Taifa Stars kucheza Mechi ya Kundi lake la kuwania kucheza Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil Mwakani dhidi ya Gambia, Timu zote 14 za Ligi Kuu Vodacom zitakuwa Viwanjani Wikiendi hii kucheza Mechi zao za tatu za Ligi.
Mabingwa Watetezi, Yanga, watasafiri kwenda huko Mbeya kucheza kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine dhidi ya Mbeya City, Timu iliyopanda Daraja Msimu huu.
Katika Mechi mbili za Ligi walizocheza, Yanga walianza kwa kuifunga Ashanti United 5-1 na kutoka Sare 1-1 na Coastal Union wakati Mbeya City walitoka Sare 0-0 na Kagera Sugar na kuifunga Ruvu Shootinga Bao 2-1.
Vigogo wa Soka Nchini, Simba, wao watacheza Jijini Dar es Salaam kwa mara ya kwanza kwenye Ligi Msimu huu kwa kucheza Uwanja wa Taifa na Timu kali ya Mtibwa Sugar, ambayo imeanza kwa ushindi na Sare kama Simba ambayo ilitoka 2-2 na Rhino Rangers na kisha kuitungua JKT Oljoro Bao 1-0.
Nao Azam Fc, ambao Msimu uliopita walimaliza Nafasi ya Pili nyuma ya Mabingwa Yanga na kuiacha Simba ikamate Nafasi ya Tatu, ipo Ugenini huko Kaitaba Stadium kucheza na Kagera Sugar.
Vinara wa Ligi, JKT Ruvu, Timu pekee iliyoshinda Mechi zake zote mbili za Ligi, watakuwa kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam Uwanja wa Azam Complex kucheza na Ashanti United ambayo imepanda Daraja Msimu huu lakini hadi sasa hali yao ni taabani baada ya kuchapwa Mechi zote mbili mfululizo.

RATIBA
Jumamosi Septemba 14
Simba v Mtibwa Sugar
Coastal Union v Prisons
Ruvu Shootings v Mgambo JKT
JKT Oljoro v Rhino Rangers
Mbeya City v Yanga
Kagera Sugar v Azam FC
Ashanti United v JKT Ruvu

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget