http://tropicalpoultryfarming.blogspot.com/

LIVERPOOL YATESA MWEZI AUGOST INCHINI EGLAND

Friday, 13 September 2013 12:59
STURRIDGE_N_RODGERS-BORA_AGOSTI>>MAMENEJA MARA NYINGI: SIR ALEX 27, WENGER 12, MOYES 10!!
>>WACHEZAJI: ROONEY, RVP, GERRARD MARA 5 KILA MMOJA!
>>REKODI: YOUNG MARA 3 MSIMU MMOJA!!
>>KLABU ILIYOTOA WACHEZAJI WENGI: MAN UNITED!
WADHAMINI wa Ligi Kuu England, Barclays, leo wametangaza waliozoa Tuzo ya Mwezi Agosti ya Ligi hiyo ya Meneja na Mchezaji Bora na wote wanatoka Liverpool.
Meneja Bora ni Brendan Rodgers na Mchezaji Bora ni Straika Daniel Sturridge.
Kwa sasa Liverpool ndio Vinara wa Ligi Kuu England baada ya kushinda Mechi zao zote 3 za mwanzo kwa Bao 1-0 katika kila Mechi na Mfungaji wa Bao zote hizo 3 ni Daniel Sturridge.
Liverpool walianza Ligi kwa kuzifunga Stoke City na Aston Villa Mwezi Agosti na Man United Mwezi Septemba.
Hii ni mara ya Pili kwa Brendan Rodgers kutwaa Tuzo hii na ni mara ya kwanza kwa Sturridge.
Meneja ambaye anaongoza kwa kutwaa mara nyingi Tuzo hii ni Sir Alex Ferguson aliekuwa Manchester United alietwaa mara 27 akifuatiwa na Arsene Wenger wa Arsenal mara 12 na David Moyes, ambae sasa yupo Man United, alipokuwa Everton mara 10.
Kwa upande wa Wachezaji, wanaoongoza kwa kutwaa mara nyingi ni Wayne Rooney, Robin van Persie na Steven Gerrard ambao wote wametwaa mara 5 kila mmoja lakini Mchezaji pekee aliewahi kuitwaa Mara nyingi katika Msimu mmoja ni Ashley Young alietwaa Mara 3 kwenye Mwaka 2009 akiwa na Aston Villa.
Manchester United ndio inaongoza kwa kutoa Washindi wengi wa Tuzo hii.
MAMENEJA WALIOTWAA MARA NYINGI:
1 Alex Ferguson Mara 27
2 Arsène Wenger 12
3 David Moyes 10
4 Martin O'Neill 8
Harry Redknapp
6 Rafael Benítez 6
Bobby Robson
8 Kevin Keegan 5
9 Sam Allardyce 4
Carlo Ancelotti
Roy Hodgson
Joe Kinnear
Gordon Strachan
14 Alan Curbishley 3
Gérard Houllier
José Mourinho
David O'Leary
Stuart Pearce

Post a Comment

Contact Form

Name

Email *

Message *

CHARLES CHAMI. Powered by Blogger.
Javascript DisablePlease Enable Javascript To See All Widget