Klabu zinazotoka katika jiji moja la Manchester zimeameangukia pua leo katika ligi kuu England. K atika dimba la Old trafod Manchester united waliwakabisha west Bromwich Albion wakapata kichapo cha magoli 2-1 wageni hao wa magharibi mwa London ndo walikuwa wa kwawnza kupata goli dk 54 kupitia kwa AMALFITANO Furaha yao hiyo ilizimwa gafla dakika tatu baadae baada ya ROONEY kusawazisha dakika ya 57 kwa mpira wa adhabu ndogo na ndipo mamchester wakawasha moto kwa kulisakama lango la west Bromwich lakini mambo yakaendelea kuwa magumu kwa man u baada ya west kufanya shambulizi la kushtukiza na BERAHINO kuiptia timu yake hiyo goli la ushindi. Katika mchezo huo watu wengi memlaumu kocha wa man u david moyes kwa kumchezesha rio fednand mechezo mingi mfulilizo baada ya leo kuonekana kuwa uchochoro kwa albion.
Tukiachana na mchezo huo majirani zao Manchester city nao wameangukia pua baada ya kupata kichapo cha magoli 3-2 dhidi ya Aston Villa man city ndo walikuwa wakwanza kupata goli kupiti kwa kiungo wao bora kabisa YAYA TOURE dk ya 45 EL AHMADI aliisawazishia timu yake dk ya 51 ya mchezo baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa bacuna iliwachukua dakika tano tu man city wakaandika goli la pili kupitia kwa mshambuliaji wao DZEKO dakika ya 56, safari hii ilikuwa BOCUNA alie kuwa mwiba mkali kwa man city baada ya kuisawazihia timu yake goli hilo dk ya 73 na kuichanganya man city na ndipo wakapata nafasi ya kuandika goli la haraka haraka dk ya 75 kupitia kwa WEIMANN mpaka mwisho wa mchezo aston villa 3 man city 2.
Nao matajiri wa London Chelsea wamewalazimisha Tottenhum hotspurs sare ya goli 1-1 mchezo huo uliokuwa wa kusisimua ulimalizika kwa timu zote mbili kugawana vipindi huku spurs wakitawala kipindi cha kwanza na kujiptia goli dakika ya 19 kupitia kwa SIGURDSSON baada kugongeana pasi safi na robato soldado. Mpaka mchezo huo unanakwenda mapumziko spurs walikuwa mbele kwa goli hilo moja, kipindi cha pili kilianza kwa kocha wa Chelsea jose mourinho kufanya mabadiliko kwa kumtoa jon obi Michel na kumwingiza JUAN MATA ndipo Chelsea walipoanza kuumiliki mchezo kutokana na mabadiliko hayo na kuweza kusawazisha goli hilo dakika ya 65 kupitia kwa nahodha wao JOHN TERRY kwa kichwa safi kutokana na mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na mata CHELEA walipata pigo baada ya mchezaji wao fernando torres kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano dk ya 81 mpaka mwisho wa mchezo spurs 1 chelsea 1 na kuifanya spurs kukwea kileleni mwa ligi kwa masaa mawili tu ikiwa na pointi 13 huku Chelsea wakishikilia nafasi ya tatu na ponti 11 Nafasi ya kwanza imechukuliwa na washika mitutu wa London arsenal kuibuka na ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Swansea city magoli ya arsenal yaliwekwa kimiani na GNABRY dk ya 58 huku goli la pili likiwekwa kimiani na mchezaji alie kwenye kiwango cha juu kabisa A.RAMSEY dk ya 62 na goli la kufutia machozi la Swansea liliwekwa kimiani na DAVIES dk ya 82 mchezo mwingine Fulhum waliwakaribisha wageni wa ligi Cardiff city na kupata kichapo cha magoli mawili kwa moja curdiff ndo walikuwa wa kwanza kupata bao dk ya12 kupitia kwa CAULKER dk ya 45 fulhum walijibu mapigo baada ya RUIZ kuisawazishia tiimu yake hiyo dakika ya 90 vijana wa MACKAY walijipatia goli la pili na la ushindi kupitia kwa MUTCH hadi kipenga cha mwisho cha mwamuzi PAWSON kinalia Cardiff city 2 fulhum 1. Wageni wengine katika ligi hiyo hull city aliwakaribisha wagonga nyundo wa London west ham united na kuwageuzia kinyundo kimoja kinyundo hicho cha hull kiliwekwa kimiani dk ya 12 na BRADY kwa mkwaju wa penati matokeo ya mwisho ya E.P.L southampon waliwakaribisha crystal palace baada ya kuwaa kuwadhibu goli mbili bila kwa magoli yaliowekwa kimiani na OSVALDO dakika ya 47 LAMBERT 49 kwa kumlipa rooney faulu nzuri .posted by charles chami
Post a Comment